Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Kocha wa Simba SC, Juma Mgunda amefanikiwa kupata ushindi mbele ya Mkufunzi wake, Hanour Janza ambaye alikuwa Mwalimu wake wa Kozi ya ukocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Hanour Janza kwa sasa ni Mkufunzi wa timu ya Namungo FC ya mkoani Lindi, Simba SC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Bao la Simba SC lilifungwa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia Moses Phiri baada ya kupokea pasi safi ya Mlinzi wa pembeni, Mohammed Hussein (Zimbwe Jr).

Kocha Mgunda alikuwa Mhitimu wa Kozi hiyo ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyodumu kwa wiki mbili mwaka 2014, Makocha waliohudhiria Kozi hiyo walikuwa 26.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...