Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kocha Mkuu wa Club Africain ya Tunisia, raia wa Ufaransa, Bertrand Merchand ameripotiwa kupata dharura ya kiafya wakati timu hiyo inajiandaa na mchezo wake wa mkondo wa pili wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) dhidi ya Young Africans SC ya Tanzania.
Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za timu hiyo, wameeleza kuwa Kocha huyo alipatwa na tatizo hilo la kiafya na kukimbizwa kwenye Kituo binafsi cha afya ili kupata vipimo na matibabu zaidi.
“Kocha Mwandamizi Bertrand Merchand amepatwa na tatizo la kiafya, na amepelekwa Hospitali kwa vipimo na matibabu zaidi, kwa hali hiyo tunamuombea Kocha wetu apone haraka na arejee uwanjani kwenye majukumu yake ya kila siku”, imeeleza taarifa hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Klabu hiyo.
Hata hivyo, Kocha huyo amepatwa na dharura hiyo ya kiafya ikiwa imebaki siku moja na saa chache kabla ya Club Africain kuwakaribisha Young Africans SC kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa mtoano wa Michuano ya CAF CC utakaopigwa kwenye dimba la Hammedi Agrebi Olympic - Redès mjini Tunis, Jumatano ya Novemba 9, 2022.
Club Africain itakuwa nyumbani huku wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya 0-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Novemba 2, 2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...