Na WMJJWM, Dodoma
Maafisa
Maendeleo ya Jamii wametakiwa kujipanga kwenda na kasi ya Serikali ili
kuchochea maendeleo ya jamii sambamba na sera, mikakati, sheria na
miongozo mbalimbali wakati Serikali ikiendelea kufanyia kazi changamoto
za upungufu wa watumishi, mazingira ya kazi na sheria ya taaluma hiyo
nyeti.
Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy
Gwajima ameyasema hayo akifungua kikao kazi cha Maafisa hao wa
Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa jijini Dodoma Novemba 08, 2022 alipokuwa akifungua
Mkutano wa Mwaka wa kada hiyo.
Dkt.
Gwajima amesema, Serikali ina matumaini makubwa na mchango wa kada hii
na itahakikisha inafanya uwezeshaji Ili kwenda na kasi iliyokusudiwa.
"Rais
Mhe. Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa sekta ya Maendeleo ya
Jamii katika kuiwezesha Jamii kushiriki kujiletea maendeleo kwa kutumia
rasilimali walizonazo hivyo kuwa kitovu cha maendeleo" na ndiyo maana
amechukua hatua ya kuunda wizara mama ya sekta hii na mambo mengi mazuri
yanakuja amesema Mhe. Dkt. Gwajima.
Akielezea
umuhimu wa kada ya maendeleo ya jamii kwenye sekta zote amewapongeza
kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuwezesha mapambano ya kutokomeza
ukatili wa kijinsia na kwa watoto huku akirejea mpango kazi wa Taifa wa
kupambana na ukatili huo kwamba serikali inakamilisha ya utekelezaji wa
miaka mitano iliyopita ili kuja na mpango mpya ambao utajibu mahitaji ya
sasa kwenye mapambano haya.
Aidha
amewapongeza Maafisa hao kwa kushirikiana na wanajamii hasa
waliojitolea kupambana na vitendo vya ukatili na kuwahamasisha wananchi
kushiriki shughuli za kiuchumi kupitia kampeni ya kijamii inayojulikana
kwa jina la SMAUJATA hali inayochangia wananchi kuwa na uelewa na
kutofumbia macho vitendo vya ukatili.
Mhe.
Dkt. Gwajima amewakumbusha Maafisa Maendeleo ya Jamii masuala
yanayotekelezwa na Serikali na kwamba wakayasimamie ambayo ni majukwaa
ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, utekelezaji wa ahadi za nchi kupitia
Jukwaa la kizazi chenye usawa ambapo Tanzani ni kinara wa eneo la haki
na usawa wa kiuchumi, programu ya malezi na makuzi ya watoto kwa kutoa
mafunzo ya malezi chanya kwa wazazi na walezi.
Mengine
ni pamoja na utekelezaji wa Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika afya
na maendeleo kwa vijana balehe, programu jumuishi ya malezi, makuzi na
maendeleo ya awali ya mtoto, usimamizi wa NGOs pamoja na uratibu wa
machinga.
Wakati huo huo, Waziri Dkt. Gwajima amezindua mwongozo wa majadiliano wa mila na desturi.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula amewataka
Maafisa hao kutimiza majukumu yao kulingana na mipango iliyowekwa na
sheria zilizopo "Maafisa Maendeleo ya Jamii, muda wa kuambiana umepita
kila mmoja asimame vema Fanyeni kazi na Wadau. Kila mnachopanga Mpange
na Wadau" amesema Dkt. Chaula.
Mwakilishi
wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Naibu Katibu Mkuu Bwana Ramadhami Kailima
amebainisha kwamba, Maafisa Maendeleo ya Jamii ndio Wasimamizi na
Watekelezaji na amewahimiza watumie Mikutano ya Mkoa na Wilaya
kuzungumzia Majukumu yao.
Akizungumza
katika kikao hicho, Mkurugenzi shirika lisilo la Kiserikali la kutetea
haki za wanawake na watoto la Kivulini Yasin Ally amesema nchi haiwezi
kufanikiwa bila kuwekeza kwenye Maendeleo ya Jamii. Amewahimiza Maafisa
Maendeleo ya Jamii kuthibitisha uwepo wao kwenye maeneo yao ambapo
ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa
Mtoto na kuwepo Mpango kazi utaowezesha kukutana na Makundi Maalum.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...