-Maporomoko yote ya maji ya Mto Ruaha yako vizuri


Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv,Njombe


WAKATI Mto Ruaha ukiwa umekauka na kuadhiri uchumi wa nchi wa mgao wa umeme na wanyama kukosa maji huku vyanzo vya maji vikiwa viko imara kwa kuwa na maji kunaacha sintofahamu maji yanakopotelea.

Hali hiyo imebainika baada ya Kituo cha Wanahabari, Watetezi, Rasilimali na Taarifa (MECIRA) na Waandishi wa Habari kutembelea vyanzo vya maji maporomoko ya Kimani-Kipengele Game Reserve na Hifadhi ya Kitulo ambapo hayo maji yanaingia kwenye mto Ruaha na kunaibua maswali juu maji yanakopotelea na kushindwa kutiririsha kwenye Mto Ruaha.

Akizungumza Afisa wa Wanyamapori wa TAWA, Kipengele Game Reserve David Titus amesema maporomoko ya kimani maji hayajawahi kupungua hata mara moja huku maporomemoko mengine yapo yanaendelea kutiririsha maji.

Amesema maji katika kipindi cha kiangazi maji kwenye maporomoko hayajawahi kupungua ikiwa kasi yake hiyo kila siku.

Mragibishi na Mdau wa Mazingira Seleman Msindi amesemq kuwa shughuli za kibinadamu ni tatizo na kusababisha mto Ruaha kuwa na ukame.

Amesema maporomoko yote yana maji yakutosha lakini mto Ruaha umebaki mabwawa bila kujua maji yanakopotelea.

Msindi amesema kuwa kiini kimeshaonekana na kutaka serikali kuchukua hatua kwa watu wanaozuia maji hayo kwa makusudi tu ili Ruaha isipate maji.





Maporomoko ya Kimani-Kipengele Game Reserve yakitiririsha maji kwenye mto Ruaha huku Mto Ruaha ukiwa umekauka.

Afisa wa TAWA wa Kipengele Game Reserve David Titus Akizungumza kuhusiana na maporomoko ya kimani yanayopeleka maji mto Ruaha yakiwa yanatiririsha maji wakati wote si kianga wala masika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...