Na.Khadija Seif,Michuzi TV
WAZIRI
wa nishati, January Makamba amewataka watanzania kutoweka vikwazo katika
kutafuta njia pekee ya kuondokana na nishati chafu badala yake watafute
njia Mbadala na kuchangia mawazo ya nini kifanyike ili kurahisisha
upatikanaji wa nishati safi na salama ya kupikia kwa Taifa zima .
Makamba
ametoa kauli hiyo leo Novemba 2 wakati akiendelea kuongoza mjadala
wa kitaifa wa siku ya pili wa nishati safi ya kupikia ambao unalenga
kuweka Sera ,sheria na mifumo mizuri itakayowezesha watanzania kupata
nishati safi .
Aidha
amefafanua zaidi kuwa ili kupata mafanikio kwa taifa zima ya upatikanaji
wa Nishati safi na Salama serikali itahakikisha Sera ,sheria na mifumo
madhubuti inawekwa vizuri huku akiwataka wadau ambao wanafikiri
kuanzisha nishati safi mbadala kujitokeza kwani atashirikiana nao katika
kutatua changamoto hiyo.
Nae
Mbunge wa jimbo la Manonga na Makamu Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya
Nishati na madini, Seif Khamis Gulamali akishiriki mjadala huo amesema
ni kilio cha muda mrefu cha Kamati na wabunge kwa ujumla na wananchi juu
ya matumizi mbadala ya Nishati.
"Ni kilio cha muda mrefu cha Kamati na wabunge Kwa ujumla na wananchi juu ya matumizi mbadala ya Nishati ya mkaa na kuni Kwa sababu tumeona madhara ambayo yanatokea katika jamii zetu.
.jpg)
"Mnapokata
Miti maana yake kunakuwepo Kwa janga la ukosefu wa mvua na njaa ambayo
inawaumiza wananchi wenyewe wananchi" Mh. Seif Khamis Gulamali, Mbunge
wa jimbo la Manonga na Makamu Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya Nishati na
Madini.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdulrahmani
Kinana akifatilia kwa kina kitabu cha yaliyomo pamoja na ratiba ya
Mjadala wa Kitaifa wa siku ya pili wa Nishati safi ya kupikia
unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere(JNICC) Jijini
Dar es salaam
Mbunge wa Jimbo la Manonga na Makamu Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya
Nishati na Madini Seif Khamis Gulamali akizungumza kuhusu mjadala wa
kitaifa wa siku ya pili wa nishati safi ya kupikia huku akiweka wazi
kuwa ni kilio cha muda mrefu kwa namna kamati yake ilikua inafanya
mchakato wa kupata nishati safi ambayo haitoathiri chochote ikiwemo
sekta ya Afya pamoja na Mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...