*DART yasema utoaji wa huduma washangaza baadhi ya nchi ya Afrika
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAKALA
wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo
haraka umekuwa kivutio baadhi ya nchi ya Afrika kuja kujifunza na
wengine kutaka nchi zao kuwa na uwekezaji huo.
Hayo
ameyasema Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa DART Deus
Kasmir kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa wakati DART walipotembelewa na
Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
waliofika kujionea huduma za usafiri wa Umma uendeshwa katika jiji la
Dar es Salaam.
Kasmir
amesema kuwa mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa sasa ndio unakuwa na
unatembelewa na mataifa mbalimbali namna wanavyoweza kutoa huduma ya
usafiri unaofanya kuchochea uchumi wa nchi kutokana wananchi kutoka
sehemu moja kwenda nyingine.
Amesema
kuwa wakati wakitembelea mifumo DART wanapata picha namna
wanavyodhibiti fedha kupitia mifumo hiyo ambapo imeonesha Tanzania
imepiga hatua kwenye mifumo ya kieletroniki kwa serikali kujua mapato
yake.
Aidha amesema kuwa
ziara ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameonesha baadhi
ya nchi kuja kujifunza na kwenda kutekeleza nchini mwao katika kutoa
huduma za usafiri wa Umma kwa wananchi.
Hata
hivyo amesema kuwa licha ya kuwa kivutio wakala unaendelea kuboresha
huduma za usafiri pamoja ba mifumo mbalimbali kutokana na teknolojia
inabadilika kila siku.
"Mradi
wa Mabasi umekuwa kivutio kazi yetu DART ni kuendelea kutoa huduma bora
kwa wananchi kwani hicho ndio kipaumbele chetu na tunasimama kwenye
hicho kipaumbele hicho"amesema Kasmir
Meneja wa Miundombinu wa DART Mhandisi Mohamed Kaganda akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Tanzania na kujifunza Huduma za Usafiri wa Umma unaotolewa na Wakala wa Mabasi Yaenday Haraka (DART,) jijinii Dar es Salaam.Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uratibu wa Sekta wa Ofisi ya Rais,Tawala za Serikali za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Enock Nyanda akikabidhi zawadi zilizotolewa na DART mara baada ya kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka na miundombinu yake kwa Makatibu Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.
Baadhi picha za Makatibu wa Wakuu wa Serikali za Mitaa wa Jumuiya ya Afrika na Watendaji wa DART wakiwa katika Basi ambalo limetumika kuonyesha mradi wa DART unavyofanya kazi wakati makatibu wa wakuu hao walipotembelea mradi huo kuona na kujifunza jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...