Na John Walter-Manyara

Vijana wenye vipaji kutoka kanda ya Kaskazini Manyara, Arusha, Kilimanjaro,Tanga pamoja na kanda ya kati Dodoma na Singida, wametakiwa kuwa wabunifu na nidhamu ili kutimiza malengo yao.

Hayo yamesemwa Novemba 14,2022 na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brand Limited David Mulokozi wakati akizindua Tamasha la kusaka vipaji linalojulikana kama (Strong Talent Search) yaliyoandaliwa na Smile FM redio pamoja na Mati super Brand Limited kupitia kinywaji cha Strong dry Gin.

Akizungumza na vijana mbalimbali kutoka mikoa hiyo waliochukua fomu za ushiriki, Mulokozi amesema kuna vijana wengi wenye vipaji lakini wanakosa sapoti na kuishia kurekodi kwa gharama kubwa kazi zao na kuziweka katika mitandao ya kijamii bila faida, lakini kupitia tamasha hilo wengi watafika mbali.

Amesema Platform hii ni fursa kubwa kwa Wasanii kwani watu wengi huwategemea katika kutuliza stress zao kwa kuburudika huku wao wakiingiza kipato.

Ameongeza kuwa kwa watakaofanikiwa kupitishwa na majaji watafundwa maadili mbalimbali ya msanii aweje na Kampuni hiyo itawasiadia kwa kila jambo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Smile Fm Redio Jamal Mteri, Mchujo wa kwanza utaanza rasmi Novemba 19, 2022 katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...