KAMPUNI ya Meridianbet
iliyoambatana na timu nzima ya masoko, akiwemo meneja masoko wa kampuni hiyo Ndugu
Matina Nkurlu, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Maudhui Bw Twaha Ibrahimu, leo
Novemba 11, 2022 ilitembelea Hospital ya Rufaa ya Tumbi mkoa wa Pwani, kwaajili
ya kutoa msaada wa vifaa kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali hiyo.
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya
Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya chini ya Waziri
mwenye dhamana hiyo Mhe Ummy Mwalimu, Meridianbet iliguswa na mahitaji ya
hospital hiyo na hivyo waliamua kuchangia neti, barakoa na vifaa vingine ikiwa
ni sehemu ya utamaduni wao wa kurudisha kwa jamii kile kidogo wanachokipata.
Meridianbet
pamoja na uongozi wa Hospitali ya Tumbi walishiriki owa pamoja katika zoezi
hilo la kukabidhiana vifaa hivyo, na mara ya kukamilika kwa zoezi la kutoa
msaada huo, mwakilishi kutoka Hospitali hiyo, Christina Salusi alitoa shukrani
zake kwa kampuni ya Meridianbet kwa msaada huo.
"Kwa niaba ya Uongozi na Menejimenti nzima ya Hospitali
ya Rufaa ya Tumbi, napenda kuwashukuru kampuni ya Meridianbet kwa kuguswa na
kuamua kutoa msaada huu mkubwa wa vifaa vya matibabu, hakika hili ni jambo
kubwa kwetu na kwa jamii nzima" alisema Christina Salusi- Muuguzi.
Aidha timu nzima ya Meridianbet walioambatana na Meneja
Masoko Matina Nkurlu hawakusita kuzungumza kile kilichowasukuma kutoa
msaada huo tena kwa mara ya kwanza kwa Hospitali ya Mkoa wa Pwani-Tumbi.
"Sisi kama Meridianbet huwa tuna utamaduni wa kutoa kwa
jamii kile kidogo tulichopata kama faida kwenye biashara yetu, na hii sio mara
ya kwanza tumewahi kufanya kwenye hospitali ya Mwananyamala, Amana n.k
“Na tumeamua kuja hapa Hospitali ya Tumbi ili kuwashika
mkono katika juhudi zenu za kuokoa maisha ya wapendwa wetu, hivyo tunawaahidi
kuendelea kushirikiana nanyi" Twaha Ibrahimu
Hata hivyo, Muuguzi ndugu Salusi alitoa nafasi ya
wawakilishibwa Meridianbet
kutembelea baadhi ya maeneo katika Hospitali hiyo ili kuwajulia hali wagonjwa
waliofika kutibiwa. Moja ya eneo
lililotembelewa ni wodi ya wajawazito ambao
nao hawakusita kutoa neno lao kwa kampuni hiyo namba moja Tanzania na Afrika Mashariki
kwa michezo ya kubashiri kutokana na msaada huo.
Mmoja ya wazazi waliojifungua katika hospitali hiyo, Bi
Zuwena Rashi mara baada ya kupokea msaada huo hakusita kuonesha hisia zake za
furaha.
"Kwakweli mimi kama mzazi nimefurahishwa na hiki
mlichokifanya kwetu, nawashukuru sana kampuni ya Meridianbet kwa kugusa maisha
yetu, hususani ya mama wajawazito na wagonjwa wengine, msaada huu utasaidia
wagonjwa wengi wanaotibiwa kwenye Hospitali ya Tumbi" -Zuwena Rashid
Kampuni ya
Meridianbet inapenda kuushukuru Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi,
Mkoa wa Pwani, kwa ushirikiano wao walioutoa mwanzo wa zoezi mpaka mwisho, na
unapongeza juhudi zinazofanywa na Hospitali hiyo kuokoa maisha ya watanzania
wengi na kurejesha matumaini zaidi. Unaweza kubeti Meridianbet kwa dau dogo la
kuanzia TZS 250/= kwa kupiga *149*10#.
Mbali na michezo ya kubashiri, pia Meridianbet wana michezo
mingine mingi ya kasino mtandaoni, unaweza kucheza mchezo wa Aviator ukawa
rubani wa maisha yako, kuna mchezo wa Roulette, Poker, n.k. Pia Kampuni
hiyo inaendesha promosheni kibao ya michezo ya kubashiri, ambapo unaweza
kujishindia Bajaji droo hii itatangazwa Novemba 22 mwaka huu, lakini pia kuna
promosheni ya SHINDA TV ya Inchi 50 kubeti kwa USSD Code.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...