Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MKOA wa Pwani umeweka mkakati wa kuwafikia wananchi nyumba kwa nyumba ,kutoa chanjo ya UVIKO-19 lengo kuongeza idadi ya watu waliochanja kufika asilimia 100 ifikapo Desemba 30 mwaka huu.

Lengo la mkakati huo ni kutoka asilimia 63 uliopo mkoa huo kwa sasa ,kiwango ambacho hakiridhishi .

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dk.Gunini Kamba alieleza hayo, wakati wa kikao cha afya kilichofanyika Mjini Kibaha kikiwa na lengo la kujadili namna ya kufikia lengo la kitaifa la asilimia 100 katika utoaji wa chanjo hiyo .

Alieleza takwimu za chanjo ya UVIKO-19 ,hadi kufikia Novemba 22 wananchi 468,187 walikuwa tayari wamechanjwa sawa na asilimia 63 lengo likiwa ni kuwafikia walengwa 757,465.

Dk Gunini alisema mkakati huo utasaidia kuwafikia wazee ambao baadhi yao kutokana na umri wao kushindwa kwenda kwenye vituo vya afya pamoja na kundi la vijana ambalo mwamko wake umekuwa mdogo.

"Kutokana na kutofanya vizuri kulinganisha na mikoa iliyofanya vizuri , tumeona fursa iliyopo kufikia Lengo ni kupata usaidizi wa kiufundi na fedha kupitia mashirika mbalimbali ya kimataifa yanayojitokeza ikiwemo WHO na Agakhan foundation"alifafanua Gunini.

Mtaalamu wa chanjo kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Caroline Akim alieleza, takwimu za dunia wagonjwa wa UVIKO-19 ni miln 6.3, vifo 6.6 chanjo zilizotolewa ni biln 12.9 na kwa Afrika miln 9.3 .

Alisema ,kwa upande wa Tanzania hadi kufikia Novemba 22 wagonjwa waliogundulika ni 38,205 vifo 845 kati ya hao 3,409 walikuwa watalaamu wa afya na kwamba chanjo milion 28.4 zimetolewa.

Akim aliongeza kuwa, mwishoni mwa wiki iliyopita wagonjwa wapya 105 waligundulika na Tanzania kwasasa imefikia asilimia 92 ya utoaji wa Chanjo ya UVIKO-19.

Nae Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Pwani Abbas Hincha alisema ,mkoa umefikia asilimia 63 ,na wilaya inayoongoza kwa jamii kujitokeza ni Kisarawe yenye asilimia 90,Kibiti asilimia 79 na Kibaha Vijijini asilimia 71 .

Alielezea kwamba, changamoto zilizosababisha kutofikia malengo ya utoaji wa chanjo ,ni muitikio mdogo wa watoa huduma za afya katika uhamasishaji na uchanjaji kwenye baadhi ya maeneo.

Hincha alitaja changamoto nyingine ni uhaba wa radilimali fedha kwa ajili ya usambazaji wa chanjo na kliniki tembezi.

Waganga wakuu wa wilaya na wakuu wa wilaya ambazo hazijafanya vizuri walieleza wanaenda kuongeza nguvu ili kufikia malengo.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...