Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd, Imran Karmal ,amepata tuzo ya kuwa Mtendaji Mkuu Bora namba 2 wa mwaka 2022 wakati wa Tuzo zilizofanyika jijini Dar es salaam.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na taasisi ya kimataifa ya KPMG kwa kwa kushirikiana na Tasisi ya Mameneja nchini Tanzania (Institute of Manager Tanzania )
Ushindi huo wa Karmal ni zawadi kwa wafanyakazi woote wa kampuni anayoiongoza ya GF Trucks & Equipment Ltd na furaha kwake kwani bila wafanyakazi imara hakuna kiongozi imara alimaliza Karmal.
Hii ni mara ya pili kwani mwaka jana alishika nafasi ya 9 kati ya CEO 100 waliokuwa wakiwania nafasi hiyo na tunashukuru mungu mwaka huu kuwa namba mbili wakati nafasi ya kwanza ikishikwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB,Abdulmajid Nsekela
Baadhi ya wafanyakazi walifurah Boss wao kuibuka kidedea kwani wanaamini mwakani katika Tuzo zinazofata ataibuka namba 1.
Karmali anaiongoza kampuni ya GF inayomiliki Kiwanda cha kuunganisha magari kilichopo Kibaha mkoani Pwani na pia ni wauzaji wa magari ya FAW,HONG YAN ambayo kwa sasa yanatengenezawa katika kiwanda kilichopo Kibaha mkoani Pwani pamoja na mitambo ya XCMG
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...