Mkutano huo umefanyika leo Novemba 25, 2022 katika ukumbi wa Kimataifa wa Julias Nyerere na kuhudhuriwa na wajumbe wa TATCA, Wajumbe wa Chama cha Waongozaji Ndege Kenya (KATCA), Wajumbe wa Chama cha Waongozaji Ndege Uganda (UGATCA), Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, wawakilishi wa vyama vingine vya usafiri wa anga Tanzania (TAISOA na TATSEA) pamoja na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUGHE Bi. Jackline Ngoda.
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa TCAA Bw. Daniel Malanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 42 wa mwaka wa Chama cha Waongozaji Ndege Tanzania (TATCA). Bw. Malanga alifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCAA.
Kaimu Rais wa Chama cha Waongozaji Ndege Tanzania (TATCA) Bw. Limis Makoloela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 42 wa mwaka wa chama hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...