WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amewataka waajiri nchini kutumia Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kuendesha mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya nchini.

Mhagama ametoa agizo hilo katika mahafali ya 36 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika kampasi ya Mtwara huku akimuagiza Katibu Mkuu wizara ya Utumishi kufuatilia na kumpa taarifa ya utekelezaji wa mafunzo kwa watumishi wapya.

"Nitoe wito kwa waajiri wote hasa ambao waraka wake utumishi uliwaelekeza kukitumia chuo hiki kuendesha mafunzo ya waajiri kufanya hivyo," amesema.

Mkuu wa Chuo hicho (TPSC) Dkt Emmanuel Shindika amesema idadi ya waajiri wanaotumia chuo hicho cha Utumishi kuendesha mafunzo elekezi kwa waajiriwa hairidhishi huku akiomba serikali kuwasisitiza waajiri kukitumia chuo hicho kutoa mafunzo kwa watumishi wapya kikamilifu.

"Idadi ya mwitikio wa waajiri kwenye taasisi, wizara na wakala za serikali kukitumia chuo cha Utumishi wa Umma kuendesha mafunzo elekezi ya awali Kwa watumishi wapya ni ndogo, " amesema.

Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 6,315 kutoka kampasi sita (Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Mbeya, Singida na Tanga) wametunukiwa vyeti baada ya kuhitimu masomo katika ngazi mbalimbali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama akiongea katika sherehe za Mahafali ya 36 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika Kampasi ya Mtwara.


Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)  ambaye pia  ni Mtendaji wa Chuo hicho Dkt Emmanuel Shindika akiongea katika mahafali ya 36 ya Chuo hicho ambayo yamefanyika katika kampasi ya Mtwara.

Sehemu ya wahitimu 6315 ambao walitunukiwa vyeti kwa ngazi mbalimbali ya masomo kutoka Kampasi sita za Chuo hicho nchini.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...