Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MBUNGE wa viti maalum wa Mkoa wa Manyara, Regina Ndege amewataka wanawake nchini wamuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ndege ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la wanawake wa jumuiya ya (UWT) wa Wilaya ya Simanjiro, kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet.
Amesema wanawake nchini wanapaswa kumuunga mkono Rais Samia kwani amefanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ya sekta ya afya, elimu, maji na mengineyo.
“Tumeona miradi mingi ya maendeleo inavyofanyika nchini, vituo vya afya vimejengwa vipya, hospitali na vituo vya afya, madarasa mapya ya shule za msingi na sekondari na miradi mingi ya maji,” amesema Ndege.
Amesema wanawake hawana namna nyingine ya kufanya kwa Rais Samia, zaidi ya kumuunga mkono katika utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ambayo inafanyika kila pembe ya nchi.
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Simanjiro Anna Shinini amesema Rais Samia amewaheshikisha mno wanawake kwa namna anavyoongoza nchi hivyo watamuunga mkono kwa juhudi zote.
Shinini amesema wanawake UWT Simanjiro watamuunga mkono Rais Samia kwa kutangaza mazuri yote anayoyafanya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...