Kazi ya kusafisha na kupima ubora wa maji katika kisima cha kwa Gwajima kinachomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Josephat Gwajima kilichopo Majengo Salasala, kata ya Goba imekamilika kwa ajili ya kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa usambazaji maji wa DAWASA ili kuboresha hali ya upatikanaji maji katika maeneo hayo.
Kisima hicho chenye urefu wa mita 47 kina uwezo wa kuzalisha lita 192, 000 kwa siku. Kazi ya uboreshaji wa kisima na kuingiza maji kwenye mfumo wa usambazaji itakamilika 18/11/2022. Kisima hiki kitatumika kuboresha hali ya upatikanaji maji kwa wakazi takribani 1400.
DAWASA sasa inazalisha jumla ya lita milioni 30.3 kwa siku kupitia visima virefu.
DAWASA inamshukuru Mhe. Gwajima kwa kujitoa na kwa kuchangia katika kuongeza wigo wa upatikanaji maji katika kipindi cha ukame
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...