Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL), jana usiku jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Hoteli ya Serena, imezindua bia mpya yenye ubora wa hali ya juu iitwayo 'Rockshore' mahususi kwa watumiaji wa hadhi ya juu na kisasa nchini Tanzania.

Rockshore, bia ya viwango vya kimataifa na inayozalishwa nchini, inakuja sokoni kama mwitikio wa hitaji la watumiaji wenye kutaka ladha mbali mbali za bia nchini Tanzania na wanaotafuta bidhaa za kipekee na zenye hadhi. Bia hiyo iliyozinduliwa pamoja na wasambazaji na wauzaji wa bidhaa za SBL ina ladha ya asili ya matunda na Pombe kwa Kiasi (ABV) ya asilimia 4.2.

Mkuu wa Uvumbuzi wa SBL, Bertha Vedastus, katika uzinduzi wa kibiashara wa bia hiyo, alisema "Tunashuhudia kukua jamii ya tabaka la kati katika makundi tofauti za umri, kutafuta upekee, mtindo na viwango vya kimataifa. SBL inawajibu watumiaji hawa kwa kuanzisha Rockshore; bia hiyo itawafanya waonekane bora zaidi"

Akizungumza katika uzinduzi huo wa kibiashara, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu Anitha Msangi Rwehumbiza alisema "Tunaendelea kusikiliza mahitaji ya watumiaji wetu yanayobadilika na kujibu ipasavyo na bidhaa tofauti zinazokidhi mahitaji hayo. Rockshore ni ubunifu nyongeza ya chapa zetu za bia"

Pia alisisitiza kuwa kinywaji hicho kinachozalishwa ndani ya nchi kitaongeza zaidi mnyororo wa thamani kwani wakulima watakuwa na soko la mazao yao kuhudumia utengenezaji wa kinywaji hiki cha kibunifu.

Uzinduzi wa Rockshore unakuja nyuma ya upanuzi wa kiwanda cha Serengeti Breweries Moshi ambayo itaendesha ujazo zaidi ili kukidhi mahitaji ya soko.

“SBL imeingiza karibu shilingi bilioni 166 katika kupanua mitambo ya kutengenezea bia katika viwanda vyote vitatu nchini (Mwanza, Moshi, na Dar) kuiwezesha kampuni yetu kuzalisha vinywaji vinavyoagizwa kutoka nje vitengenezwe ndani kama vile Rockshore na Captain Morgan Gold, ambayo huongeza thamani katika msururu wa usambazaji” Anitha Msangi Rwehumb aliongeza.

Wadau mbalimbali wa sekta ya vinywaji na burudani wamepokea ingizo jipya la Rockshore kwa mwitikio mzuri. Nancy Sumari, mlimbwende na mshindi wa tuzo ya Miss Tanzania (2005), aliongezea kwa kusema “ NInafuraha sana hii bia ya Rockshore sasa inatengenezwa Tanzania. Ni suala zuri sana sababu linakuja mstari wa thamani Tanzania kwa kutengeneza ajira kwa vijana, kuwawezesha wakulima na watu mbalimbali watakao husika katika usambazaji wa bidhaa hii”.

Bia ya Rockshore inakuja sokoni ikiw ana historia ndefu yenye kuakisi uzoefu wa kuburudisha kutokea anga za Magharibi Pwani ya Ireland, kutoa mguso wa kigeni kwa watuamiaji wa hadhi ya juu.

Rockshore itapatikana kote nchi na bei ya rejareja inayopendekezwa ya Tshs 2,500.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...