Na Janeth Raphael MichuziTv - Dodoma.

Katika utekelezaji wa Program ya utoaji Elimu wa masuala ya Fedha Serikali inakusudia ifikapo mwaka 2025 takribani asilimia 80 ya wananchi watakuwa wamepata uelewa wa masuala ya Fedha.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dodoma alipokuwa akitoa maelekezo kuhusu wiki ya huduma ya Fedha kitaifa Kamishna uendeshaji wa sekta ya Fedha Charles Mwamwaja kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara alisema kuwa Kutokana na Utafiti wa FinScop wa mwaka 2017 Nchini ni asilimia 48.6 tu ya nguvu kazi ndiyo waliotumia huduma rasmi za fedha na hivyo kubaki na kundi kubwa la watanzania ambao hawafaidiki na huduma hizo.

"Hivyo kukosa fursa za kuboresha maisha yao kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi na hatimaye kuchangia katika kukuza Pato la Taifa,"alisema.

Aidha amesema kuwa malengo ya wiki ya huduma za fedha ni pamoja na kujenga uelewa na weledi kwa umma katika matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa ili kujenga uchumi na kuondoa umaskini.

Na Kuimarisha ufanisi wa masoko ya Fedha kupitia elimu ya Fedha,kuongeza upatikanaji wa huduma za fedha,kutoa elimu ya kuwezesha kumlinda mtumiaji wa huduma za kifedha,kuwezesha wananchi kusimamia vizuri Rasilimali fedha

"Kuwezesha wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na matumizi sahihi ya huduma za fedha katika kukuza biashara zao,kuimarika kwa Utamaduni wa kujiwekea akiba,kukopa na kulipa madeni pamoja na kuongezeka kwa mchango wa sekta ya Fedha kwenye ukuaji wa uchimi,"alisema.

Amesema kuwa wiki ya huduma za fedha inalenga kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa umma, wanafunzi,wakufunzi,wanawake,vijana,watu wenye mahitaji maalum,wajasiriamali wadogo na wakati(SMEs),asasi za kiraia,wahariri na waandishi wa vyombo vya habari,watoa huduma za fedha,watoto na ummakwa ujumla.

Maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa ni utekelezaji wa Mpango mkuu wa mendeleo ya sekta ya Fedha wa mwaka 2020/21-2029/30,elimu kwa umma ni moja ya maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wa Mpango huo.

Wizara ya fedha na Mpango imeandaa programu ya kutoa elimu kwa umma ya mwaka 2021/22-2025/26 programu hiyo imeweka mikakati ikiwa ni pamoja na matukio na mbinu mbalimbali zitakazotumika katika utoaji wa elimu ya Fedha kwa umma.

Kauli mbiu itakayotumika katika wiki ya huduma za fedha kitaifa ni "Elimu ya Fedha kwa maendeleo ya watu".
Kamishina wa idara ya maendeleo ya Sekta ya fedha Dkt Charles Mwamwaja akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...