Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akitoa maelekezo baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa sekondari mpya ya mfano ya Joseph Kizito katika Kata ya Lituta Ha;mashauri ya Madaba ambapo serikali imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akikagua jengo la utawala na vyumba nane vya madarasa katika shule ya sekondari Josseph Kizito Halmashauri ya Madaba ambapo serikali kupitia mradi nwa SEQUIP imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo ambao umefikia asilimia 95 Mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kata ta Kizuka Halmashauri ya wilaya ya Songea ambao umegharimu shilingi milioni 470 fedha ambazo zimetolewa na serikali kupitia mradi wa SEQUIP Baadhi ya majengo ya utawala na vyumba vya madarasa katika shule mpya ya sekondari Luhira Manispaa ya Songea ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP kwa gharama ya shilingi milioni 470.

********************

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejenga shule mpya 11 za sekondari mkoani Ruvuma zilizogharimu shilingi bilioni 7.7.

Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Mipango katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankoo amezitaja shule hizo mpya kuwa zimejengwa katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma.

Amesema shule hizo zimejengwa kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP) ambapo kila Halmashauri imejengwa shule moja kwa thamani ya shilingi milioni 470.

Hata hivyo amesema katika Halmashauri ya Tunduru zimejengwa shule tatu za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP na kwamba katika Halmashari ya Namtumbo pia zimejengwa shule mbili ikiwemo shule ya wasichana ya Mkoa iliyojengwa katika eneo la Migelegele kwa gharama ya shilingi bilioni tatu.

“Mradi wa SEQUIP umewezesha kila shule ya sekondari kuwa na jengo la utawala,vyumba vya madarasa, vyoo,mfumo wa maji, maabara,maktaba na jengo la TEHAMA ,shule zote zinatarajia kuanza kuchukua wanafunzi Januari 2023’’,alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amekagua moja ya shule hizo katika Halmashauri ya Madaba.

Akitoa taarifa ya mradi wa shule hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amesema mradi wa ujenzi umetengewa shilingi milioni 470 na ulianza utekelezaji Machi 2022 ambapo hadi sasa fedha zilizotumika ni zaidi ya shilingi milioni 468.

Amesema ujenzi wa mradi huo upo katika hatua za ukamilishaji ambapo hadi sasa umefikia asilimia 95 ukihusisha ujenzi wa madarasa nane,jengo moja la utawala,vyumba vitatu vya maabara,matundu 20 ya vyoo,minara miwili ya matanki na mfumo wa kunawa mikono.

Hata hivyo amesema ujenzi upo katika asilimia 65 kwa majengo mawili ambayo ni jengo la maktaba na chumba cha TEHAMA na kwamba mradi unatarajia kukamilika kwa asilimia 100 kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemwagiza Mkandarasi kushughulikia dosari zote zilizojitokeza ikiwemo mipasuko kwenye kuta.

Amesema Rais ametoa fedha nyingi kutekeleza mradi huo hivyo ni lazima majengo yalingane na thamani ya fedha kwa kutekeleza mradi katika ubora na viwango.

Katibu Tawala wilaya ya Songea Pendo Ndumbaro ameahidi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi ambapo amemwagiza Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamlisha mradi huo.

Serikali inatekeleza mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa kujenga shule mpya za sekondari 1000 katika nchi nzima.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Novemba 27,2022

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...