Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amesema Wilaya ya Songea inatarajia kukamilisha ujenzi wa madarasa yote 96 yanayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.9 ifikapo Novemba 30 mwaka huu.
Akizungumza na Menejimenti ya Mkoa ikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Ndugu Stephen Ndaki katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Songea,Mheshimiwa Mgema amesema ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari unaendelea vizuri ambapo wanatarajia kumkabidhi madarasa yote Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ifikapo Desemba 10 mwaka huu.
Ameitaja Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuwa imepewa shilingi bilioni 1.5 kujenga madarasa 76 ukilinganisha na Halmashauri za Songea ambayo imepewa milioni 200 kujenga madarasa 10 na Madaba pia imepewa shilingi milioni 200 kujenga madarasa 10.
Wilaya ya ya Songea inaundwa na Halmashauri tatu ambazo ni Manispaa ya Songea,Halmashauri ya Madaba na Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Imeandikwa na Albano Midelo
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Novemba 21,2022.
Baadhi ya madarasa yakiwa katika hatua za ukamilishaji Manispaa ya Songea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...