Kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi ya Knauf
Gypsum Tanzania imesema mazingira ya uwekezaji hapa nchini yameboreka
kwa kiasi kikubwa na kutangaza kuwekeza shilingi bilioni 115 katika
upanuzi wa kiwanda chake kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Kampuni
hiyo yenye asili ya Ujerumani tayari imeshawekeza kiasi cha shilingi
bilioni 163 hapa nchini kwenye kiwanda na uzalishaji wa vifaa mbali
mbali vya ujenzi wa nyumba ikiwamo gypsum na imesema itawekeza kiasi
kingine cha shilingi bilioni 115 kufikia mwaka 2025.
Akiongea
wakati wa halfa ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ajili ya
kuwashukuru wateja wake na wadau mbali mbali, Mkurugenzi wa Knauf ukanda
wa Afrika Mashariki Ilse Boshoff aliishukuru serikali, wateja na wadau
mbali mbali kwa kuifanya safari ya uwekezaji wa kampuni hiyo hapa
Tanzania yenye mafanikio.
Kila kunapokucha kampuni ya Knauf
inapiga hatua kadhaa mbele. Historia yetu kwa hapa Tanzania ilianza
mwaka 2014 tulipofungua ofisi na baadaye kuanzisha Kampuni ya Knauf
Gypsum Tanzania na kuanza kazi rasmi mwaka 2017,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alifafanua kuwa mwaka 2018 kampuni hiyo ilianza ujenzi wa kiwanda
cha kisasa kilichopo Mkuranga mkoani Pwani na mwaka 2020 kilianza
uzalishaji kikiwa na uwezo wa kuzalisha mita za mraba milioni 15 kwa
mwaka.
Akitangaza uwekezaji zaidi katika kiwanda hicho
alisema.,“Uwezo wa uzalishaji kwa kiwanda cha Mkuranga ni mita za mraba
milioni 15 kwa mwaka na malengo yetu ni kukipanua na kukiwezesha
kuzalisha mita za mraba milioni 43 kwa mwaka kufikia mwaka 2025.
Uwekezaji huu utagharimu shilingi bilioni 115,”
Aliongeza kuwa
upanuzi huo utakifanya kiwanda hicho kuwa kikubwa kuliko vyote kwa
Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na pia utakifanya kiweze kuongeza
usafirishahi wa vifaa inavyozalisha nje ya Tanzania kwa asilimia 170.
Dickson
Mtekere, mmoja kati ya wateja wa Knauf aliyehudhuria hafla hiyo kutoka
kampuni ya Shananga Group Limited ya Dar es Salaam aliishukuru Knauf
kwa kuweza kuwakutanisdha wateja wake na kutambua mchango wao katika
kuongeza soko la bidhaa zinazotengenezwa kwa malighafi za Kitanzania
zikitumia teknalojia ya kisasa kutoka nchini Ujerumani.
“Naishukuru
Knauf kwa kutukutanisha wateja wake na kutambua mchango wetu. Uwekezaji
wa kampuni hii umetusaidia sana sisi wafanyabiashara kwa kuwa
wanatengeneza bidhaa ambazo kabla ya kuja kwake tulilazimika kuziagiza
nje ya nchi kwa gharama kubwa huku tukipoteza muda mwingi. Ni wazi kuwa
upanuzi wa kiwanda cha Mkuranga utaongeza fursa za kibiashara na ajira
kwa Watanzania,” alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania inajishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi Ilse Boshoff (kulia) na meneja masoko wa kampuni hiyo Lilian Mangaru (kushoto) wakimkabidhi mkurugenzi wa kampuni ya Super Terrazzo Ltd Nish Hiran tuzo baada ya kuibuka mshindi wa usambazaji wa bidhaa za kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania inajishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi Ilse Boshoff (kulia) akimkabidhi cheti mwakilishi wa duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Shanoga Hardware la Dar es Salaam Anna Kijugu cheti ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa duka hilo katika kuuza bidhaa za ujenzi zilizotengenezwa na malighafi za ndani zinazotengenezwa na kapuni hiyo. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko (Marketing manager) wa Knauf Lilian Mangaru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania inajishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi Ilse Boshoff (kulia) akishuhudia Meneja masoko wa kampuni hiyo Lilian Mangaru (kushoto) akimkabidhi tuzo mmoja wa wateja wa kampuni hiyo Dickson Mtekere kutoka kampuni ya Shananga Group Limited ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutambua wa kampuni hiyo katika kuuza bidhaa za ujenzi zilizotengenezwa na malighafi za ndani na kampuni ya Knauf.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...