Na Said Mwishehe, Michuzi Blog
NOVEMBA 10 mwaka huu nimebahatika kuwa mmoja ya Watanzania tulioungana na raia wa mataiafa mengine kushiriki Kongamano la Sanaa ni Biashara ambalo limefanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa kukumbusha tu Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni moja ya matukio makubwa ambayo yamefanyika kuelekea kwenye Tamasha kubwa la muziki na Sanaa linaloabdaliwa na Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Hivyo kwenye kongamano hilo wadau mbalimbali wa Sanaa nchini wameshiriki na kisha wakatoa maoni na ushauri kuhusu sanaa ya Tanzania kuitoa ilipo na kuipeleka kuwa Sanaa yenye faida,Sanaa inayolipa wasanii wa Tanzania .Mada Kuu ilikuwa inasema Sanaa ni Biashara.
Wengi wamechangia mada huyo, maoni mengi yametolewa, ushauri na kila aina ya maelezo yenye lengo la kuhakikisha Wasanii wa Tanzania wanapiga hatua za kinaendeleo umetolewa .Hakika ni Kongamano kubwa na waandaaji walijiandaa.Hongera zao .Ujue kwenye kongamano hilo nimewaona wasanii wengi na maarufu.Nimekutana na Wasanii wa kipindi kile.Hata Suma G aliyetambana na wimbo Vituko Uswahilini alikuwepo.
Najua unakumbuka , Hivi ni Vituko Uswahilini , Ulikuwa wimbo uliotamba sana ,basi kwa ukubwa na umuhimu wa kongamano hilo Suma G akaona hataki kuahadithiwa bora afike na asikie kwa masikio yake.Hata Mike T alikuwepo na nakumbuka alitamba na nyimbo zake nyingi lakini kichwani kwangu nakukumbuka wimbo uliokuwa unasema ' Mnyalu Sitabadilika' .
Yaani waliokuwepo wasanii wengi hata dada yetu Starah Thomas naye alikuwepo.Wamefika kusikiliza maoni ya wadau wa Sanaa wanasema nini.Ushiriki wa wasanii ulikuwa mkubwa sana, hata Taff G wa East Coast naye alikuwepo .Hapo sijaamua kutaja orodha ndeefu ya wasanii wa filamu ,Sanaa ya ngoma asili na wengi wengiiii.Kulikuwa kitamu mnoo.
Basi bwana pamoja na maoni mengi kutolewa na wadau wa sanaa ndani na nje ya Tanzania binafsi nilivutiwa na kuusikiliza ujumbe wa Katibu Mkuu Wizara ya Michezo,Sanaa na Utamaduni Dk.Hassan Abbas. Alitoa ujumbe huo alipokuwa anahitimisha Kongamano hilo.
Wakati anaanza kutoa ujumbe wake Dk.Abbas alianza kwa kueleze ukubwa wa tamasha la 41 lakimataifa la Sanaa na Utamaduni ambalo linafanyika kwenye Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). "Na kama mnavyofahamu ni mwaka wa 41 tumekuwa na tamasha hili lakini tunaendelea kuliboresha na tunaahidi tutaendelea kuikukuza na kuitangaza Bagamoyo lakini liitangaze Tanzania , katika miaka 41 ijayo tunaamini tamasha hili litakuwa kubwa zaidi.
"Niwashukuru watoa mada maana hawa ndio watu adhimu kwa siku ya leo , hawajatunyima ujuzi, tumekuja kujifunza, kusikiliza , hivyo ni wajibu wetu kunyonya ujuzi wao.Watoa mada wote wamebobea kwenye sekta ya Sanaa, wanaijua na waniishi.Wametufundisha, tumefundishika.
" Tumekuja kujifunza namna ya kuchukua sanaa yetu kwenda kwenye bishara,kujiondoa tulipoo kwenye malalamiko kwenda kwenye mafanikio, tumekuja kwenye Kongamano hili kujifunza namna ambavyo wenzetu duniani ambao tunawatajataja majina wametoka kwenye malalamiko wako pale wanatengeneza fedha ingawa wengine wanaharibu hizo fedha.
" Lakini kongamano hili limetusaidia kuanzisha mjadala mpana zaidi namna gani wasanii Watanzania watatoka kuwa wasanii maarufu lakini masikini kwenda kuwa wasanii wa Tanzania ni maarufu lakini matajiri wenye fedha, hiyo ndio dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan lakini ndio dhamira ya Wizara yetu.
Dk.Abbasi amesema wamekuwa wakiweka mipango, mikakati, mbinu na wakati fulani ikibidi wanapambana vita kwa ajili ya wasanii wa Tanzania huko nje ya kuhakikisha wasanii wetu wanakwenda kimataifa, wanakwenda kutengeneza fedha , hiyo ndio azma waliyonayo.
Amesema hivi karibuni wanajiandaa kwenda Siato kuwapambania wasanii wa Watanzania."Lakini tutakwenda mpaka kule Dalas kwenda kuwapigani wasanii watanzania kutengeneza fursa na majukwaa.Hatuendi huko kutafuta malalamiko, tunakwenda kutafuta mafanikio.
"Kwa hiyo kongamano la leo liwe muendelezo na sio mwanzo wa watanzania kuona tunatokaje, sio unajua ilikuwaje jana mimi nilikosa Shoo.Kwa hiyo uendelee kukosa Shoo? Tengeneza thamani upate Shoo zijazo na ndicho ambacho Serikali tunafanya.
"Mimi kwenye kongamano hili nimeona mambo saba na nitaja baadhi ya mambo.Jambo la kwanza Wasanii wawe na mipango na malengo, kimezungumza kitu kinaitwa Identity tujaribu kutengeneza Identity zetu kama umekaa kenye hip hop nata na biti sio umekaa kwenye Hip Hop imekuja singeli.
"Unasema na mimi ngoja nijaribu , singeli ikishuka unasema ngona nirudi kwenye taarabu, huna Identity , kwa hiyo imejitokeza sana kwenye kongamano hili.Lakini wasanii wetu hawasimami kwenye malengo yao , wapo wenye malengo lakini ndio hayo sasa akisikia kitu fulani kime-trend kishaacha malengo yake na yeye ana anatrend kule.
"Kwa hiyo linakuwa Taifa la wasanii wanaotrend lakini hawana muziki mzuri, mashairi wala hawana pafomasi nzuri, kunapokuwa na matamsha makubwa duniani huendi, huwezi kwend Tamasha la Kochela kule South Califonia , huwezi kwenda kuimba kwa kiki, uzabizabina, kiroho papo kwenda kuimba huwezi, huwezi.
"Msanii wa Tanzania kutumia Kadabraa, uzabizabina na ukiroho papo kwenda kwenye tamasha kama Tomorrow Land kwa kule Poland. Huwezi msanii wa Tanzania kufanya makikiki yetu na blaa blaa zetu hizi kwenye tamasha kama Rio Festival watu million nne ndani ya wiki moja wanashriki kwenye hilo tamasha."
Katika kuendelea kutoa ushauri,maoni, Mapendekezo kuhusu Sanaa ya Tanzania kuwa biashara Dk.Abbas akawa anazungumza laini lakini iliyokuwa inapenya kwenye mioyo ya wasanii, watalaamu wa sekta ya Sanaa.
Anaelezea kwamba kwa hiyo kwenye kongamano hilo la Sanaa ni Biashara wamejifunza zaidi mambo ya kuzingatia ili kwenda kibiashara.Pia amesisitiza hili nimelikumbha wakati wanajadili Sanaa ni Biashara wamejifunza kuhusu maadili.
"Huwezi kusema mimi ni msani, kwa hiyo ukiwa msanii inakuaje? Ndio unakuwa tapeli,ndio huvai vizuri? Si ndio? Yaani ukiwa msanii ndio blaa blaa nyingi? Ndio kila siku Meneja mpya , ndio usanii huo? So ndio! Hujakamilisha dili ya biashara unameneja mpya, kuna mmoja alimkataa hadi meneja mwenzie, inapigwa simu anamkataa mwenzie.
"Ndugu zangu hii sanaa lazima tuwe Verry Smart kuipeleka mbele, la sivyo tutabaki tu kulalamika Shoo hakuna, muziki wetu sio mzuri, mjomba yule aliyenikataza nisafanye muziki wakati niko shule ya msingi ndio kanitia laana.Kumbe ni wewe mwenyewe matendeko yako ,silka na hulka yako hazikufanyi muziki wako na sanaa yako kuwa biashara.Dhana ya maadili hata sisi kwenye Wizara inategemewa kuwa nguzo kubwa sana."
Aidha Dk.Abbas anaelezea kwenye kongamano hilo kuwa anafikiri na ndio ukweli Rais Samia anakuwa Rais wa kwanza kwenda kwenye Tamasha la Hip Hop la msanii mkongwe Joseph Mbilinyi maarufu Sugu.Anathamini sana na yeye naamini tumuombee kheri ,afya njema atazidi kwenda kwenye matamasha mengi ya sanaa.
"Lakini sio kwenda tu Rais anatutuma kama nilivyosema Mheshimiwa Waziri, Katibu Mmendaji na Mimi Katibu Mkuu tunachokibali kwenda kwenye tuzo za Afrima Dalasi.Tunakwenda Siato na huko kote ni kupiga Kingereza tu kuwatetea wasanii wa nchi hii ya Tanzania, kwa hiyo wewe umekaa tu mtandaoni hujapost wiki mbili, ukipost meza imejaa sasa wewe tukusaidiaje.
"Maana shughuli zako zote hazioneshi wewe tukupe shughuli gani ya kufanya.Yaani wewe tunajaribu kupambana kwa ajili yako msanii halafu mwenyewe hata huna habali.Ni kweli msanii tunakujua lakini tukusaidie vipi kwenye sanaa yako? Maana kila unachotuonesha hakiendani na sanaa, kuvaa hovyo ndio usanii?
" Kujaza meza ndio usanii? Kama ndio usanii basi tuendelee na hiyo . Jambo jingine la kusisitiza ni kuhusu brand , wasanii wetu wengi brand hakuna lakini kujiongeza .La mwisho katika kufanikiwa sote tumtegemee Mwenyezi Mungu, tusingefika hapa bila Mwenyezi Mungu.Msanii mwaka mzima hujawahi kuwambia Mungu ahsante , halafu unakuja unasema ooooh sera hakuna,Shoo sipati, hela kwenye sanaa hakuna wakati Mungu hujawahi kumshukuru , hujaenda kumsifu bwana.
Ameongeza Dk Abbas kwenye mafanikio sio tu kwenye sanaa , hata wao makatibu wakuu , mkuu wa wilaya wanapata muda wa kumshukuru Mungu."Unaweza kuwa Bise lakini Mungu ukimshuru naye anashtuka yuko Mwishehe anatoka Michuzi, Mungu anakumbuka, wewe unaomba Shoo lakini hujaomba Shoo kwa Mwenyezi Mungu, unaomba shoo kwa Mapana , unaomba Shoo kwa DC wa Bagamayo Mungu hajakushukia
"Kwasababu anaangalia huyu kweli anataka Shoo kwa Mapana na Mapana mwenyewe kawezeshwa na Mungu.Mimi sio Sheikh wala Mchungaji lakini nawahusia wote, wasanii wanahabari sote tupate nafasi ya kumshukuru Mungu, asilimia kubwa tunayopanga na kutamani yeye ndio anapanga, unaweza kuwa na mipango mizuri, malengo mazuri lakini usipompa nafasi, usipotoa nafasi ya kiroho kidogo huwezi ukafanikiwa,"amesema Dk Abbas
Baada ya kuzungumzia hayo kwa mapa na marefu ndani ya muda mfupi akatumia nafasi hiyo kueleza aneona ayaseme hayo kwa Wasanii wake wa Tanzania kupitia Kongamano hili."Niseme Kongamano la mwaka huu nimelifunga hadi kwenye kongamano lingine mwakani,mada na muda utaelezwa wakati ukifika kwa sasa tukale na usiku tukutane kwenye siku ya kwanza ya tamasha la 41 la Sanaa na Utamaduni linalofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ( TaSUBa).
Kaphone
0713833822
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea zawadi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyochorwa na wanafunzi wa TaSUBa kabla ya kufungua rasmi Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo Novemba 11, 2022 ambalo linafanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mkoani Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea zawadi ya picha yake iliyochorwa na wanafunzi wa TaSUBa kabla ya kufungua rasmi Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo Novemba 11, 2022 ambalo linafanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...