Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, (TIA) Profesa William Pallangyo akizungumza wakati akifungua semina ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa taasisi hiyo ambayoitawasaidia kuanziisha biashara mbalimbali watakapomaliza masomo yao. Semina hiyo ya siku moja ilifanyika leo katika Taasisi hiyo Kampasi ya Singida.
.Mratibu wa Ujasiriliamali , Imani Matonya akizungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa wanafunzi hao.
Wanafunzi wakishiriki kwenye semina hiyo.

Mratibu wa Ujasiriamali na Kituo Atamuzi wa Kampasi ya Singida , Mohamed Kaluse (kushoto) akiwa na mratibu mwenzake kutoka Dar e Salaam wakati wa semina hiyo.
Wanafunzi wa Taasisi hiyo wakiwa kwenye semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Uhasibu Tanzaia (TIA), Kampasi ya Singida imetoa semina kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kupunguza changamoto ya upungufu wa ajira inayowakabili vijana wengi pale wanapomaliza masomo yao ya elimu ya juu.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) , Prof. William Pallangyo amesema semina hiyo ya Ujasiriamali itawasidai vijana hao kuanziisha biashara mbalimbali watakapomaliza masomo yao.
Pallangyo alisema hayo wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Taasisi hiyo ya Uhasibu Tanzania namna ya kubuni mawazo mbalimbali ya biashara, yatakayowasidia kujiajiri wenyewe na kuacha tabia ya kusubiri kuajiriwa.
Alisema kumekuwa na ufinyu wa ajira katika sekta mbalimbali hivyo kupitia mfunzo hayo ya ujasiriamali itasaidia kutambua fursa zilizopo.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu- Taaluma, Dk. Momole Kasambala alisema Taasisi ya Uhasibu Tanzania imejipanga kutoa mafunzo hayo mara kwa mara kwa ajiliya kuwajengea uwezo wa kupata mawazo ya biashara ambayo yatawasiadia katika kujiajiri.
Aidha Dk.Kasambala alisema wanafunzi wenye mawazo mazuri watashindanishwa na mawazo yatakayoshinda yatapelekwa mbele zaidi kwa kutafutiwa mitaji na kukutanishwa nataasisi za kifedha ili wanafunzi hao waweze kupata mikopo ya kuanzisha biashara.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yatawasidia kuanzisha biashara zitakozowasaidia kuondokana na changamoto ya upatikananji wa ajira.
Wamesema kupitia biashara hizo pia wataweza kuajiri vijana wengine ambao hawana ajira na hivyo kuwasaidia vijana wengi waliomaliza vyuo na hawana ajira kupata ajira nchini.
Hata hivyo wameomba taasisi za kifedha kuweka mikopo yenye riba nafuu ambayo itawasiadia wao kukopa na kuanzisha biashara ambazo zitatoa ajira kwa vijana wengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...