Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kaimu Afisa Habari wa Klabu ya Azam, Hashim Ibwe amesema kuwa nchini Tanzania hakuna timu ambayo haitaki huduma ya Kiungo Feisal Salum (Feitoto) ambaye kwa sasa anacheza katika Klabu ya Yanga.
Ibwe amesema hayo wakati akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya Simu, amesema kuwa bado hawajafungua mazungumzo na Feisal lakini amethibitisha na wao Azam FC wanahitaji huduma ya Kiungo huyo machachari.
Ibwe amesema licha kuwa hakuna mazungumzo kati ya Azam FC na Kiungo huyo, amethibitisha tajiri wa Klabu hiyo, Yusuf Bakhresa amesema muda wowote hakuna shida kuhusu kuipata huduma ya Kiungo huyo.
Kupitia kurasa wake rasmi wa ‘Instagram’ Ibwe amendika, “Kumbe hizi Rangi za Buluu Buluu zinapendeza eenh na hiviiiii pale Chamazi kwani jezi namba 6 anavaa nani?”.
“Hakuna timu isiyotaka huduma yako Feisal Salum na sisi Azam FC tunaitaka pia tajiri kasema muda wowote hakuna shida makubaliano tu”.
Feisal amekuwa kwenye kiwango bora katika nafasi ya Kiungo katika Klabu ya Yanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...