Na Mwandishi wetu

Turaco Collection Tanzania imepiga kambi katika maonesho ya kimataifa ya wasafiri (WTM) mjini London, Uingereza ili kuuza na kutengeneza mtandao wa kuuza vivutio vya Tanzania na uwezo wake wa kusafirisha watalii katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Maonesho hayo ya 43 yaliyoanza Novemba Saba hadi Novemba 9 hutumika kwa ajili ya kutangaza mambo yanayohusu usafiri na utalii.

Kampuni na mashirika yenye majina makubwa kwa kawaida kuhudhuria mkutano huo ambao hutengeneza mtandao wa mawasiliano kuhusu utalii na usafiri.

Mkutano huo hutumika kubadilishana mawazo na kusaidia wataalamu wa utalii na usafiri kutengeneza uzoefu wa hali ya juu wa namna ya kuhudumia wasafiri na watalii.

Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata akiziwakilisha hotel zao katika maonesho hayo ya WTM London anasema kwamba, maonesho hayo ni eneo jema kabisa la kujitangaza kubadilishana uzoefu hasa katika dunia ambayoi walaji (watumiaji wa huduma) wamekuwa wakibadilika kutokana na mazingira yanayotokea duniani.

Alisema wamefika katika maonesho hayo ya 43 yanayofanyika ExceL London kuona namna ambavyo wanaweza kujiuza kwawatalii mbalimbali duniani na kutambulisha bidhaa zao ikiwamo safari mbalimbali na mahoteli wanayoshughlika nayo.

Turaco Collection kwa upanded wa utalii wa kaskazini pamoja na bidhaa mbalimbali za utalii pia wana; Ngorongoro Valley Lodge na Manyara View Point Lodge. Kwa Zanzibar wana Doubletree Reasort by Hilton Nungwi, Doubletree by Hilton Stone Town na Beyt Aly Salaam-By Turaco.

Kwa Dar es Salaam wana Element By Westin Marriott na Delta By Marriott.

Turaco wana mipangilio kadhaa ya Safari za kitalii zinazopangwa kwa uangalifu ikiwamo safari katika mbuga za kusini za Tanzania na wiki moja Zanzibar. Unaanza safari hiyo katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere kwa kukaa kwa siku tatu kwenye Ziwa Manze, kambi ya msituni katika eneo la ufuo wa ziwa lenye wanyama pori karibu na tawi la Mto Rufiji, kisha utaelekea magharibi zaidi hadi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kukaa kambi ya Mdonya Old River , ukiangalia tembo wanaotembelea kambi hiyo mara kwa mara.

Baada ya hapo utakwenda Zanzibar na kukaa katika hoteli ya kifahari iliyo katikati ya Mji Mkongwe na kujifunza historia ya kuvutia. Kituo chako cha mwisho kwenye sampuli hii ya safari ni Doubletree Nungwi Beach Resort katika ufuo mzuri wa mashariki wa Zanzibar, ambapo unaweza kuruka juu ya miamba ya matumbawe yenye rangi nyingi au kupumzika tu ufukweni na kujianika juani!

Florenso Kirambata akizungumza alisema soko la usafiri duniani linahitajio dunia kuungana tena ili kukuza mitandao yao ya biashara, kuchunguza mienendo na kuweka mikataba muhimu.

Maonesho hayo yanatarajiwa kutembelewa na zaidi ya wageni 30,000 .
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata (kulia) na washirika wenzake, Mkurugenzi wa Antelope Safaris, Rose Abdallah na Meneja Mauzo na Masoko wa Serena Hotels, David Sem (kushoto) wakiwa katika maonesho ya usafiri na utalii (WTM) mjini London, Uingereza. Turaco ni kampuni ya utalii nchini inayomiliki pia hoteli kadhaa.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata katika maonesho ya usafiri na utalii (WTM) mjini London, Uingereza jana. Turaco ni kampuni ya utalii nchini inayomiliki pia hoteli kadhaa. (Picha naTuraco)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...