Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

KUNA changamoto kubwa ambayo Sasa hivi kama taifa tunaipitia inayotokana na ukame mkubwa uliosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Zile habari za mgao wa umeme kutokana na kina Cha maji kupunguza kwenye mabwawa yetu ya kuzalisha umeme kama Mtera,Kidato Ruaha zimerudi tena .

Taarifa za mgao wa maji zimerejea na hata mito iliyokuwa inapeleka maji kwenye mabwawa hayo za kuzalisha maji katika miji kadhaa ikiwepo Jiji la Dar es Salaam .

Siku za karibuni Kamati ya mawaziri nane wakiongozwa na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeeo ya Makazi Dk.Angelina Mabula wamekuwa kwenye ziara ya kutembelea mikoa na Wilaya mbalimbali.

Walipofika Mto Ruaha wamekuta Mto huo hauna maji kabisa, ukame umekuwa mkubwa na ukiongeza na shughuli za kibinadamu ndio kabisa Mto Ruaha ni moja ya mto unaopeleka maji yake kwenye mabwawa yetu yanayozalisha umeme.

Hata Bwawa la Mwalimu Nyerere Rufiji moja ya chanzo Cha maji yake yanatoka Ruaha.Hali ni mbaya, sio poa kabisa.

Katika ziara hiyo ya mawaziri nane ambayo pamoja na mambo mengine ilitoa elimu wananchi kuacha shughuli za kibinadamu kando ya mito mikubwa ambazo zinaharibu mazingira.

Naibu Waziri wa Nishati Byibato ambaye alieleza kwa kina kuhusu mito inayopeleka maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme.

akaweka wazi maji ya kwenye mito hiyo inahitajika na kila mmoja wetu kwa shughuli mbalimbali lakini kwenye nishati ya umeme wanategemea sana uwepo wa mito hiyo kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme wa maji ambayo gharama yake ya uzalishaji Iko chini ukilinganisha na vyanzo vingine kikiwemo Cha kutumia mitambo inayoendeshwa kwa mafuta mazito.

Kwa bahati mbaya wakati ukame ukiendelea kupiga hodi katika kila kona ya nchi yetu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetoa utabiri wake unaonesha mvua zitakuwa chache kwa mwaka huu Kumbuka hata utabiri uliotolewa kwa Septemba,Oktoba na Novemba nao ulipnesha kuwa na mvua chini ya wastani au wastani na sasa utabiri unaotupeleka Desemba na kuendelea unaonesha kutakuwa na kiasi kidogo Cha mvua .

Kwa lugha rahisi huu ukame utaendelea, tutaendelea kukosa mvua na hivyo maji yataendelea kupungua ama kukauka kabisa kwa mito tunayoitegemea .Kama hali itakuwa hivyo nini kifanyike? Hapa majibu yatakuwa mengi ya nini kinapaswa kufanyika.Nchi yetu inayo wataalamu wa kutosha hivyo watashauri.

Binafsi kwa mtazamo wangu wa kawaida naona kabisa umefika wakati kwa nchi yetu kuwekeza kwenye vyanzo vya umeme ambao utatokana na na nishati jadidifu.Tuwekeze kwenye umeme jua, maana jua lipo la kutosha na kwa utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonesha hakutakuwa na mvua nyingi.

Maana yake jua litakuwa lipo tena jua Kali na kutosha.Tufikirie umeme jua .Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameonesha namna umeme jua unavyoweza kusaidia kukabiliana na mgao lakini kwa muda mrefu amekuwa akiamini umeme unaotokana na nishati ya gesi asilia unaweza kuwa wa uhakika zaidi.

Kwa nchi kama za China na India wao wameamua kujikita katika umeme unaotokana na jua, wamefanikiwa sana wanapata umeme wa kutosha ambao unatumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi .

Kwa Tanzania tunapaswa pia kuelekea huko,tuweke nguvu zetu kwenye kuanza kutengeneza vyanzo vya umeme unaotokana na jua.Natambua vyanzo vya maji ni muhimu,tunavyo na tutaendelea kuvitumia lakini hiyo haina haana tusiitumie vyanzo vingine.

Nchi yetu tunayo maeneo mengi yenye upepo mwngi na unaokwenda kwa Kasi, nao inatosha kabisa kutumika kama chanzo mojawapo Cha kuzalisha nishati ya umeme, ndio hivyo Sasa kama maji ambayo tumekuwa tukiyatumia yameanza kukauka tufanyeje.Tusubiri mvua ambayo hatujui inanyesha lini tufikiria nishati jadidifu inayotuzunguka .

Nafahamu tunayo miradi ya umeme unaotokana na upepo kama kule Singida lakini Wizara ya Nishati nadhani Iko haja ya kuweka nguvu zaidi.Tukaribishe wawekezaji kama tutaona inafaa,wawekeze kwenye kuzalisha umeme wa upepo, wahitaji tupo tutaitumia.


Ukiondoa jua,upepo na maji, nchi yetu tunayo maeneo yenye maji moto maarufu zaidi kwa jina la Jotoardhi, ni miongoni mwa vyanzo vya kuaminika vya kuzalisha umeme.

Tutumie vyanzo hivyo ili tuwe na umeme wa uhakika .TANESCO kwa sasa mbali na mambo mengine wamekuwa wakitoa ratiba ya mgao wa umeme, na sababu kubwa ni kupungua kwa maji kwenye mabwawa.

Kwa mtazamo wangu tuweke nguvu na kwenye vyanzo vingine vya nishati, tuliweka nguvu kwenye chanzo Cha maji pekee yake huko mbele ya Safari tunaweza kuingia kwenye wakati mgumu.

Lakini tunayo gesi asilia ya kutosha huko mikoa ya Kusini ,ni kweli tunao umeme unaotokana na gesi asilia basi Serikali Ione haja ya kuwekeza kwenye eneo hilo pia, sio vibaya tukawa na umeme mwingi unaotokana na gesi .

Tunayo mitambo pale Kinyerezi inayozalisha umeme unaotokana na gesi, Serikali iangalie namna ya kutumia gesi asilia kuhakikisha umeme unaozalishwa unakuwa wa kutosha na hivyo kupunguza ukubwa wa tatizo.

Nafahamu Serikali unajua zaidi kuliko akina sie lakini kwa kuwa Serikali yetu ni sikivu isikie na hiki ninachoeleza.Huenda nimeeleza kwa juu juu wao wanaweza kuboresha .Na kama sijaeleweka basi washike tu maneno mafupi ya kwamba Tanzania tutumie nishati jadidifu kukabiliana na mgao wa umeme.

Shirika la Haki Madini pamoja na mambo mengine kwa muda kumekuwa likiitazama nishati jadidifu kama njia sahihi ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na mbadiliko ya tabia nchi , naunga na Ha Madini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihamasisha wataalamu walioko Serikali kuona haja ya kutumia Nishati jadidifu katika kuzalisha umeme,kutumia nishati jadidifu katika uendeshaji wa shughuli za viwandani.

Haki Madini wamekuwa na matumaini makubwa na nishati jadidifu iwapo tunataka kuona tunaondoka a na athari za mabadiliano ya tabianchi.Kwenye umeme hakika nami naungana na Haki Madini kusisitiza kwa hali ilivyo hasa ya huu ukame suluhu na uhakika wa umeme ipo kwenye nishati jadidifu mtaani tunaitaga nishati mbadala.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...