Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Ward Holdings Tanzania (WHT) imesafirisha tani 8 za korosho zilichakatwa kwenda soko la Marekani hatua muhimu itakayoosaidia kukuza biashara na kuongeza hamasa kwa wakulima sambamba na kuinua pato la taifa kupitia tasnia ya korosho.

Akizungumza katika hafla ya kusindikiza mzigo wa kwanza wa kihistoria kusafirishwa kutoka Tanzania kwenda moja kwa moja katika soko nchini Marekani jana, Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo ,Bw Anthony Mavunde alisema hatua hii ni kubwa katika kukuza sekta ya zao la korosho hapa nchini.

“Hiki tunayoshuhudia hapa ni dalili njema kwa wakulima wa zao hili la korosho ikiwa ni miongoni mwa zao lenye mchango mkubwa kwenye mazao yanayoingizia taifa fedha za kigeni”, Alisema Bw. Mavunde.

Aliongeza kuwa, “Sehemu ya biashara hiI ni matunda yatokanayo na jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua uhusiano mzuri na Masoko ya nje ya nchi.

Aidha, Bw. Mavunde amebainisha kuwa mpango wa serikali ni kuwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 60% ya korosho iwe inabanguliwe hapa nchini jambo ambalo litachagiza ujenzi wa viwanda vingi vya kubangua korosho vitakavyozalisha ajira nyingi kwa watanzania.

“Ni mpango ambao sisi kama Wizara tumejielekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 tuwe na viwanda vya kutosha ambavyo vitabangua korosho kwa asilimia 60% nah ii itafungua ajira nyingi kwa vijana wetu”, Alisema Bw. Mavunde.

Kwa upande wake Rais wa kampuni ya WHT Bw. Godfrey Simbeye mbali ya kumshukuru Waziri Mavunde kukubali kuja kushuhudia tukio hilo, amesema korosho hizo zitasafirishwa moja kwa moja kwenda nchini Marekani kwa ndege na kubainisha kuwa kampuni hiyo imekua kampuni ya kwanza kuratibu tukio hilo huku pia akiweka wazi matarajio yao ni kusafirisha tani laki mbili na nusu kwa mwaka.

“Tukio hili kwetu kama WHT ni tukio zuri lenye taswira nzuri kwa wazalishaji wa korosho kwani uhitaji wa zao hili kwenye masoko ya nje ni mkubwa na sisi kwa kuliona hilo tumeanza na tani 8 lakini malengo yetu hasa kwa mwaka huu ni kusafirisha tani laki mbili na nusu”, Alisema Bw. Simbeye.

Bw. Simbeye alitumia fursa hio kuwahimiza wakulima hasa wazalishaji wa korosho kuhudumia mazao yao vizuri ili korosho inayozalishwa nchini iendelee kuwa na ubora ambao unaifanya iitajike kwenye soko la dunia.

“Mimi ninapenda nitoe wito kwa wakuima wetu wazidi kujikita kwenye uzalishaji wa zao hili kwani matunda yake ni makubwa na mahitaji pia ni makubwa kwenye masoko ya nje”, Alisema Bw. Simbeye.

Aidha Bw. Simbeye aliweka wazi kuwa sehemu ya mzigo huu unaosafirishwa utakuwepo kwenye maonyesho yajulikanayo kam TANZA-FESTIVAL yatayofanyika nchini Marekani kuanzia tarehe 4 mpaka 6 mwezi wa huu.

Naye mwakilishi wa Balozi wa Marekani nchini Bw. Robert Adrian Raines amesema tukio hilo limekua sehemu ya ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo.

“ Haya ni matunda mazuri ya ushirikiano mzuri kati yetu nah ii inataleta ustawi mkubwa kibiashara na kilimo na italeta tija kwa wakulima wa zao la korosho.



Naibu waziri wa Wizara ya kilimo, Anthony Mavunde (kulia), akisindikiza mzigo wa kwanza wa Tani 8 ya korosho iliyobanguliwa na Kampuni ya Ward Holdings Tanzani(WHT) ikisafirishwa kwenda soko la Marekani kwenye hafla iliyofanyika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Lengo likiwa kukuza biashara, kuongeza hamasa kwa wakulima na kukuza pato la Taifa kupitia tasnia ya korosho. Nyuma ni Mwakilishi wa Balozi wa Marekani, Bw. Robert Raines na Kulia ni Rais wa Kampuni WHT, Bw. Godfrey Simbeye.


Rais wa Kampuni ya Ward Holdings Tanzania (WHT), Bw. Godfrey Simbeye, Akizungumza kwenye hafla ya kusindikiza mzigo wa kwanza wa kihistoria wa Tani 8 ya korosho iliyobanguliwa kusafirishwa kutoka Tanzania kwenda soko la Marekani iliyofanyika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu waziri wa Wizara ya kilimo, Anthony Mavunde.  Kushoto ni  Mwakilishi wa Balozi wa Marekani, Bw. Robert Raines.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...