Na Mwandishi Maalumu-Lagos,Nigeria
UBALOZI wa Tanzania, nchini Nigeria umeendelea na mkakati wa kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya 'Tanzania The Royal Tour'.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutangaza Tanzania kupitia sekta ya utalii nchin.
Hayo yamethibitika Oktoba 3, mwaka huu, baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, ulipoandaa onesho maalimu ya filamu hiyo kwa wadau wa utalii wa nchi za Uwakilishi za kituo hicho.
Maonesho hayo yalifanyika sambamba na maonesho ya Utalii ya 18 ya Akwaba, jijini Lagos, Nigeria, ambapo zaidi ya washiriki 500 walishiriki maonesho hayo, na makampuni 30 yalikuwa yakionesha bidhaa zake za utalii vikiwemo vivutio vya utalii wa matibabu.
Aidha, Makampuni matano ya Utalii kutoka Tanzania yalishiriki na kupata fursa ya kukutana na wadau wa utalii wa soko la Afrika Magharibi.
Home
UTALII WETU
Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria waipaisha TANZANIA THE ROYAL TOUR soko la utalii la Nigeria, Afrika Magharibi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...