UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe umeonesha kuwa wafanyabiashara ndogondogo wanapata unyanyasaji kutoka katika Mamlaka mbalimbali katika kutafuta maeneo ya kufanyia biashara.
Akizungumza wakati wa Kusambaza matokeo ya Utafiti huo leo Novemba 12, 2022 jijini Dar es Salaam kwa Wafanyabiashara wa Mbezi na stendi ya Magufuli, Mtafiti kutoka Chuo hicho, Aloyce Gervas, amesema kuwa Utafiti uliofanywa na chuo Kikuu Mzumbe kuanzia Mwaka 2017 katika Sekta ya Usafirishaji na wafanyabiashara ndogo ndogo juu ya kujipatia huduma za hifadhi za jamii umeonesha kuwa Wafanyabiashara ndogondogo wanashindwa kufanya biashara zao kwa uhuru kwasababu hawana maeneo ya kufanyiabiashara.
Amesema kuwa zaidi ya Asilimia 71 ya wafanyabiashara hao hawana namna ya kupata mikopo kwa kuwa hawana maeneo rasmi ya Kufanyiabiashara na hawaaminiki kwasababu kila siku wanabadilisha maeneo ya Kufanyia biashara zao.
"Hiyo inawapa changamoto katika kujipati vipato vyao vya kila siku."
Gervas amewaomba Mamlaka kuanzia Serikali za mitaa ambapo wafanyabiashara hao wanafanyia biashara waweke utaratibu rasmi na kuwatengenezea maeneo rasmi ya biashara ili waweze kukidhi mahitaji yao.
Amesema kama Mamlaka zikifanya hivyo wafanyabiashara watakuwa na staha na Serikali inaweza kujua Idadi ya wafanyabiasha ndogondogo waliopo kwa kupitia Serikali za Mitaa na makundi mbalimbali ambayo watakuwa wamejiunga katika maeneo hayo.
"Serikali inaweza kupata mapato kupitia wafanyabiashara hao endapo tuu hawatakuwa na hali ya kukimbizwa kimbizwa wanapofanya biashara zao katika maeneo rasmi yanayokuwa yamepangwa na Serikali."Amesema Aloyce
Akitolea Mfano wa jinsi wafanyabiashara wa Coco Beach walivyopangwa amesema kuwa pale hamna migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wafanyabiashara na Mamlaka kwa sababu wamepangwa vizuri.
Kwa Upande wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo Amesema Mamlaka mbalimbali na Serikali itambue kuwa Wafanyabishara pia wanaona namna ambavyo wafanyabiashara wa Coco Beach walivyoboreshewa maeneo yao ya kazi hivyo ameomba Mamlaka ziweze kuwaboreshea na wafanyabiashara ndogo ndogo.
Dkt. Kinyondo amesema kuwa wafanyabiashara hao bado hawajapata ya hifadhi ya jamii na bima ya afya kwa sababu kati ya wafanyabiashara 200 waliopata Matokeo ya Utafiti uliofanyika ni watu wawili tuu ndio wanabima ya Afya na kati ya hao Mfanyabishara mmoja ndio anachangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Amesema kuwa Wafanyabiashara ndogondogo hawana elimu juu ya Bima ya Afya na juu ya Uchangiaji wa mifuko ya Pensheni ingawa wanauwezo wa kupata kiasi cha shilingi 20, 20000 kwaajili ya kuchangia katika mifuko hiyo kwa kila mwezi.
Pia amewaomba wafanyakazi katika mifuko ya Pensheni na Bima ya Afya watoke maofisini waende kutoa elimu kwa wananchi juu faida na kujiunga kwenye mifuko hiyo ili kuondoa utegemezi wakati mtu akiugua au kuzeeka.
"Wajitokeze kwenye Mitaa ili Watu wengi waweze kupata elimu juu ya huduma wanazozitoa na taarifa walizonazo kwaajili ya wafanyabiashara ndogondogo taarifa hizo zisiishie Ofisini tuu." Amesema Dkt. Kinyondo
Kwa Upande wa Amani Mwinyimkuu amesema kuwa kwa wafanyabiashara wa stendi ya Magufuli na Mbezi amesema wamefanikiwa katika kuunda vikundi mbalimbali lakini hawajafikia hatua ya kutimiza malengo ya makundi yao.
Amesema kuwa Vikundi vingi vimesajiliwa lakini wanashindwa kupata hifadhi za jamii na bima ya afya kwa kuwa wanafuata Mkumbo hivyo elimu zaidi iendelee kutolewa ili waweze kujiunga na mifuko hiyo kwaajili ya manufaa yao ya sasa na baadae.
"Tumeona Uelewa ni Mdogo, kwahiyo nashauri, Vikundi vingi vinahitaji elimu ya hali ya juu. "
Utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 68 wamejiunga na Vikundi asilimia 32 hawajajiunga na kikundi chochote na Asilimia 23 wamejiunga na Mifumo rasmi ya hifadhi za Jamii kama NSSF.
Kwa Upande wa Mfanyabiashara, Rems Lutumo amewaomba Chao Kikuu Mzumbe kuwafikishia taarifa Mamlaka juu ya Maeneo ya Hifadhi za Barabara ambazo zinamaeneo makubwa kuwatengenezea Vibanda Rasmi wafanyabiashara hao ili waweze kujipatia kipato.
"Serikali inajenga Barabara hii ya Kutoka Mjini Kuelekea Mlandizi kunamaeneo ya Road Reserve yaliyobakia makubwa tuu ambayo kwa sasa Serikali haitumii kwa lolote, tungeomba Watafiti mchukue maoni ya wafanyabiashara ndogondogo hawa kwamba, Maeneo yote ambayo yapo karibu na Vituo vya daladala badala ya kukodisha Mtu mmoja mmoja nae akodishe watu Serikali ijenge Mabanda ya kisasa ya muda ili wafanyabiashara hawa wafanye biashara katika maeneo hayo." Amesena Lutumo
Amesema kuwa hapo watakuwa wamewawezesha wafanyabiashara hao kutoka hatua moja kwenda Nyingine kuliko kufukuzana kila kukicha.
Pia wamepewa viakisi mwanga ambavyo vinaujumbe na Namba za simu za watu wa Mikopo, Bima ya Afya na Mfuko wa Pensheni ambazo zitawawezesha kujipatia fursa mbalimbali.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara ndogondogo wenye umri zaidi ya miaka 50 wa stendi ya Magufuli na Mbezi jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na wafanyabiashara ndogo ndogo wa Stendi ya Mafuguli na Mbezi jijini Dar es Salaam wakati wa kusambaza Utafiti.
Mfanya biashara Elizabeth Richard akilalamikia jinsi Bima zinavyowasilisha michango yake kwenye hospitali na jinsi wanavyochangia kukosekana kwa huduma za Afya wa watu wenye Bima za afya.
Mfanyabiashara, Rems Lutumo akizungumza wakati wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakisambaza matokeo ya Utafiti juu ya wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii na Bima ya Afya.
Amani Mwinyimkuu akitoa elimu juu ya kujiunga na vikundi mbalimbali ambavyo vitawasaidia kupata baadhi ya huduma kwa Urahisi.
Wafanyabiashara mbalimbali wakisikiliza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo na Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa Stendi ya Magufuli na Mbezi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...