Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana ameelekeza wanawake kutunza misitu ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababisha upungufu wa maji katika meneo mbali mbali nchini.

Ili kuunga mkono pia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa misitu na mazingira,Waziri Chana amekabidhi mitungi ya gesi 108 kwa baadhi ya wanawake wa Jumuiya ya wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Njombe itakayoweza kusaidia kupata nishati katika shughuli zao na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa niaba ya wanawake wilayani Njombe,mwenyekiti wa jumuiya hiyo Beatrece Malekela wakati akikabidhi mitungi hiyo amesema wanawake wa wilaya ya Njombe wapo tayari kuendelea kuunga mkono juhudi za wizara na serikali katika utunzaji wa misitu na mazingira.

“Tunashukuru kwa Mhe Waziri kuendelea kutoa hamasa kwa wanawake ili watumie gesi na hizi ni juhudi za kumuunga mkono Mh,Rais kama alivyoanza kumtua mwanamke ndoo kichwani lakini pia sasa ni kumtua mwanamke mzigo wa kuni kichwani,sisi tutaendelea kuunga mkono”amesema Beatrece Malekela.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...