Meneja wa Ubunifu wa Costech, Dk. Athman Mgumia akizungumza na waandishi wa habari jiji ni Dar es Salaam mara baada ya warsha ya siku mbili ya wadau wa ubunifu  mara baada ya kubadirishana uzoefu na kutengeneza mahusiano yatakayowawezesha kuendeleza bunifu zao kiteknolojia.
baadhi ya wadau wa Ubunifu wakiubadirishana uzoefu na kutengeneza mahusiano yatakayowawezesha kuendeleza bunifu zao kiteknolojia.

KATIKA kuhakikisha teknolojia ya ubunifu inazidi kukua na kuleta tija kwenye jamii, wadau mbali mbali wa bunifu katika masuala ya kilimo, fedha na elimu wamekutana kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 3, 2022 Meneja wa Ubunifu wa Costech, Dk. Athman Mgumia amesema katika warsha hiyo ya siku mbili, wadau hao watabadirishana uzoefu na kutengeneza mahusiano yatakayowawezesha kuendeleza bunifu zao kiteknolojia

Dk. Mgumia amesema mpango huo unaoratibiwa na Kitengo cha ubunifu cha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ni ushirikiano baina ya nchi za Bara la Afrika na zile za Bara la Ulaya.

Amesema mpango huo ni jukwaa la fursa kwa wajasiriamali kupanua wigo wao hasa kwenye eneo la ubunifu wa kiteknolojia ambapo wabunifu hao sasa wataweza kushirikiana katika kuendeleza bunifu zao kwenye maeneo ya teknolojia ya kilimo, miamala ya fedha na elimu.

Amesema, Jukwaa hilo ni kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kushirikiana katika fursa kwa wajaasiriamali na wadau teknolojia ya Kidigitali waliopo nchini Tanzania na wale waliopo katika nchi nyingine za Afrika na kule barani Ulaya.

Ametaja lengo lingine ni kutoa fursa kwa wajasiriamali na wabunifu kuanzisha mahusiano ya kimkakati katika kuendeleza bunifu zao za kijaasiriamali walizozianzisha kwa kupata uzoefu kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika na nchi za Ulaya.

Amesema kuwa jukwaa hilo pia linaendeshwa sambamba na majukwa mengine yanayoendelea kwenye nchi nyingine kama vile la Uganda, Ghana na Nigeria kwa Afrika na Italia kwa upande wa Ulaya.

Naye Rose Funja, Mbunifu wa Teknolojia ya drone (ndege nyuki kwenye kukusanya takwimu za kilimo na Mawasiliano, amesema kuwa wanatumia teknolojia hiyo kukusanya picha na taarifa mbalimbali kupitia mionzi inayoonekana kwa macho na ile isiyooneka kwa macho kwenye kilimo na kuitumia kujua mimea ina afya kiasi gani.

Ameongeza kuwa pia wanaitumia teknolojia hiyo katika kuwashauri wakulima kwa sababu inaonyesha mimea ipi imeharibika.

Amesema tayari washafanya mradi wa Kilimanjaro Agriculture Devolpment kwenye shamba la Mpunga ambapo walitumia drone na kukusanya taarifa na kuwashauri wakulima juu ya matokeo ya data hizo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ubinifu na Atamizi wa Chuo Kikuu cha Sayansi Mbeya (MUST), Justine Mwakatobe amesema katika warsha hiyo amejifunza namna ya kutumia teknolojia hususani ya drone kwa upande wa elimu na kilimo

"Ujuzi nilioupata hapa nitakwenda kuwasaidia wabunifu waliokuwa chuoni kwetu kwa sababu chuoni kwetu tunawabunifu," amesema Mwakatobe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...