Na Mwamvua Mwinyi,Pwani


WAKUU wa wilaya mkoa wa Pwani wamesaini mkataba wa usimamizi wa lishe ,ambao watapaswa kuusimamia utekelezaji wake kwa kipindi cha miaka minane ili kupunguza vifo na udumavu kwa watoto .

Mkataba huo ni hatua ya kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ambapo watapaswa kusimamia utekelezaji kwa kipindi hicho.

Akiwasainisha mkataba huo ,mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge aliwaeleza, baada ya hatua hiyo ,watatakiwa kufanya muendelezo wa kuwasainisha mikataba wakurugenzi wa halmashauri zao kisha kushuka ngazi za chini hadi mitaa.

Alisema mikataba hiyo ina viashiria 14 vya utekelezaji ambavyo vinatakiwa kusimamiwa kutoka 10 vya awali.

“Mkataba huu una viashiria 14 vya utekelezaji ambavyo watendaji wanapaswa kuvisimamia ikiwemo kutenga pesa kiasi cha Sh.1,000 kwa kila mtoto mwenye umri wa miaka mitano ili zitumike kwa lishe maeneo ya shuleni,” alieleza Kunenge.

Viashiria vingine ni asilimia ya sampuli za chumvi kutoka kwenye kaya zilizokusanywa kupitia wanafunzi na kupimwa uwepo wa madini joto.

“Tutawapima juu ya asilimia ya shule za msingi na sekondari zinazotoa chakula shuleni,” Matokeo ya kazi hii yatapimwa kwa vitendo na kuona kama yaliyomo kwenye mkataba yanatekelezwa ,na Kama hayatatekelezwa sitosita kuchukua hatua kulingana na kanuni zilizopo"alifafanua Kunenge.

Nae Mganga Mkuu Mkoani Pwani, dkt.Gunini Kamba alieleza,hali ya lishe inaimarika tofauti na miaka ya nyuma, jambo ambalo limetokana na juhudi za wataalamu wa lishe kutoa elimu kwa jamii.

“Baadhi ya wazazi walikuwa na mwamko mdogo juu ya lishe bora wakiamini kuwa vyakula kama chipsi mayai ndio lishe bora, jambo ambalo siyo bali hata mbogamboga pia ziko kwenye kundi la lishe,” Gunini anasema.

Gunini alifafanua kwamba, baada ya hatua ya kusaini mkataba huo, matarajio ni kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga 11 kati ya vizazi hai 1000 ambavyo vilikuwepo kwenye ripoti ya mwaka 2021.

Hata hivyo,wataalamu wa afya wameshauriwa kuelekeza nguvu kwenye kutoa elimu ya lishe ndani ya jamii ili kuzalisha vizazi bora.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...