Zawadi zenye thamani ya Sh.
Mil. 10.5 za droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’
zimepata wenyewe mwishoni mwa wiki, ambapo washindi 76 walipatikana, 75
kati yao wakijishindia fedha kiasi cha Sh. Mil. 7.5, huku Asumwisye
Stallone akiibuka na zawadi ya bodaboda yenye thamani ya Sh. Mil. 3.
Kampeni
hiyo, ambayo inaendeshwa na Benki ya NMB kwa ushirikiano na Mastercard
International, ikilenga kuhamasisha matumizi ya NMB Mastercard kufanya
malipo, Lipa Mkononi kwa kuskani QR na kufanya malipo mtandaoni huku
zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350 zitatolewa
katika miezi mitatu ya kinyang’anyiro hicho.
Akizungumza kabla
ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa NMB, Manfredy
Kayala, alisema malengo makuu ya kampeni hiyo iliyoanzishwa mwaka 2018,
ni kuihamasisha jamii katika kuachana na matumizi ya pesa taslimu
‘cashless’, lakini pia ikilenga kurejesha sehemu ya faida yao kwa wateja
wao.
Kayala alifafanua kuwa, ukiondoa bodaboda moja na pesa
taslimu kwa washindi 75 wa kila wiki, NMB MastaBata Kote Kote itatoa
zawadi kwa washindi 49 wa droo za mwisho wa mwezi, sambamba na bodaboda
mbili, na droo ya fainali itazawadia safari za Dubai kwa washindi na
wenza wao kwa siku nne.
Mbele ya Ofisa wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania (GBT), Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam,
Donatus Richard, alisema NMB MastaBata Kote Kote ni muendelezo wa benki
yake katika kuwafanya wateja na Watanzania kugeukia utamaduni chanya wa
matumizi yasiyohusisha pesa taslimu.
Alifafanua kuwa, MastaBata
Kote Kote inagusa wateja wote wa ndani na nje ya nchi wanaotumia kadi za
Mastercard au Lipa Mkononi kaa kuscan QR na kutoa wito kwa Watanzania
kuhakikisha wanatumia kadi zao katika kufanya malipo na miamala
mbalimbali ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda.
Kampeni hii
ya NMB MastaBata KoteKote itaendelea kwa takribani miezi mitatu.
Kutakuwa na washindi wa kila wiki, kila mwezi na na wale wa Grand
Finale. Wateja wanapaswa kufanya malipo kwa kadi Ya NMB Mastercard au
Lipa Mkononi (mastercard QR) ili kujiwekea nafasi ya kushinda.
Meneja
wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, akibonyeza kitufe cha
kompyuta kuchezesha droo ya kwanza ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote
Kote’ inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la
Mlimani City, Deogratius Kawonga na Kulia ni Meneja Mwandamizi Idara ya
Kadi na Biashara wa NMB, Manfredy Kayala.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...