Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha


MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha,Mussa Ndomba amewaasa baadhi ya watendaji wa mitaa na kata waache kukaidi kukusanya baadhi ya ushuru kwenye vyanzo vya mapato badala yake watimize wajibu wao ili kuiondolea hasara halmashauri .

Amemtaka ofisa utumishi kuwaandikia barua ya kuwakumbusha wajibu wao na kuwafuatilia na endapo wakiendelea kukaidi basi wawajibishwe kwa kuchukuliwa hatua stahiki.

Akizungumza na baadhi ya watendaji wa mitaa na kata waliofika kuhudhuria baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Ndomba aliwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea .

"Kuna watendaji wasumbufu, hawataki kutimiza wajibu wao wakiona upande wa kukusanya ushuru sio jukumu lao , wengine hawakai ofisini kila ukienda ofisini kwao huwakuti , kwenye ukusanyaji ushuru hawapo ,tusibembelezane,wapo vijana wengi wanahitaji nafasi hizo"

"Kwasasa ukiingia katika 18 zetu umeumia, watu wanajiona wapo juu ya halmashauri,Leo iwe mwisho , watendaji msifanyekazi kwa mazoea ,mnajali kazi zenu kuliko kazi kuajiliwa , haiwezekani atakaeona hawezi kuendelea au kutekeleza majukumu aliyoajiriwa kuyafanya aache "alisisitiza Ndomba.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mshamu Munde,alisema watendaji wanapaswa kusimamia mapato yatokanayo na vibali vya ujenzi.

Alieleza ,watu wanajenga ,": Lakini hakuna makusanyo yoyote yanayokusanywa ,hivyo watendaji wa mitaa ni wajibu wao kushiriki kukusanya mapato hayo ili kuinua mapato ya halmashauri.

Awali diwani wa kata ya Pichandege Karim Mtambo alieleza ,ofisi za kata hazijapata ruzuku miezi sita sasa ,wamekuwa wanyonge kwani fedha hizo zinacheleweshwa.

Akijibu hoja hiyo mweka hazina wa Halmashauri hiyo (TT) , Nicholas Haraba alisisitiza japo wanahitaji ruzuku Lakini watendaji hao wamekuwa hawakusanyi ushuru wakati ni wajibu wao.

"Changamoto ni ukusanyaji wa mapato ,wanapaswa wafuate muongozo wa ajira yao ili walipwe ruzuku na asilimia 5 ya makusanyo"alieleza Haraba .

Alitaja vyanzo vya mapato wanavyopaswa kusimamia watendaji wa mitaa na kata na kukusanya mapato ni sanjali na ushuru wa mchanga,ujenzi,magulio na ushuru wa soko.

"Ni hasara kulipa watu wengine ,kuwaajiri na kuwalipa wakati jukumu la kwanza la watendaji hawa ni kukusanya mapato"alifafanua .

Haraba alibainisha kwamba ,ruzuku zao zipo kwenye mchakato wa taratibu ziweze kutoka ili walipwe Lakini kubwa wanapaswa kutimiza wajibu wao pasipo kupuuza.

Kwa upande wake ,ofisa utumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Protas Dibogo ,alisema tayari kuna zaidi ya milioni nne zipo kwa ajili ya kulipa wiki hii ili kuendesha ofisi zao.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...