Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
HALMASHAURI
ya Mji wa Kibaha, Mkoani Pwani, imekadiria kukusanya sh. bilioni 45.8
kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato yake katika kipindi cha robo
ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Akisoma
taarifa ya bajeti kwenye kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika
Mjini Kibaha, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina Wilson
amesema kuwa bajeti hiyo ya fedha ni ya Julai hadi Septemba mwaka huu.
Selina
ameeleza ,fedha hizo zinatokana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
ruzuku, mapato ya ndani na washirika wa maendeleo wa Halmashauri hiyo.
Amefafanua,hadi
sasa makusanyo yaliyopatikana katika kipindi cha robo mwaka kuanzia
Julai hadi Septemba kiasi cha fedha kilichokusanywa ni shilingi milioni
8.4 sawa na asilimia 18 ya makusanyo kwa kipindi hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...