Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley (kushoto), pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo toka kwenye Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika Mkutano wa mwaka wa tathmini ya utendaji sekta ya uchukuzi uliofanyika jijini Dar es salaam.

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ametembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililopo katika maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa lengo la kutangaza kazi za taasisi mbalimbali zilizopo chini ya wizara hiyo.

Maonesho hayo yamefanyika leo Novemba 16, 2022 katika ukumbi wa Kisenga LAPF - Dar es salaam, wakati wa mkutano wa 15 wa wadau wa kutathmini utendaji kazi wa sekta ya uchukuzi kwa mwaka mmoja.

Mbarawa akiambatana na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Africa (AFDO) Dkt. Patricia Laverley, wameelezwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa kwa sekta ya ujenzi na uchukuzi ikiwa ni pamoja na huduma mahususi za usafiri wa barabara, maji na anga.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Wilbert Muruke amewataka wananchi kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya hewa hasa katika sekta ya uchukuzi ili waweze kutekeleza majukumu ya sekta vilevile kukabiliana na athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa.

“Kama mnavyoelewa huduma za hali ya hewa ni mtambuka kwa sekta mbalimbali mojawapo ya sekta ambayo tunaihudumia ni sekta ya usafirishaji ambapo katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo viwanja vya ndege, reli, barabara na madaraja moja ya taarifa muhimu katika mipango yao ni taarifa za hali ya hewa zitakazowawezesha kupanga vyema mipango yao na hivyo kusaidia kuepusha hasara zitakazojitokeza kutokana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa”. Amesema Muruke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...