Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za mwisho kwa miili ya watu waliopata ajali ya ndege  ya shirika la Precision  , iliyotokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji waliojitokeza kuaga miili ya watu waliopata ajali katika ndege ya shirika la Precision, iliyotokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Miili ya marehemu waliofariki katika ajali ya ndege ya Shirika la Precision iliyotokea Novemba 6, 2022, ikiwa imewekwa katika eneo maalum kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera kwa ajili ya kuagwa na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu katika maombolezo yaliyofanyika kweye uwaja huo Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Ndege ya Shirika la Precision iliyopata ajali Novemba 6, 2022 ikiwa pembezoni mwa uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuvutwa kutoka eneo la ajali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpongeza na kumfariji kijana Jackson Majaliwa kwa ushujaa wake wa kuwahi katika eneo ilipotokea ajali ya ndege ya Shirika la Precision na kuwaokoa abiria waliokuwa wameshindwa kutoka ndani ya ndege hiyo. Maombolezo ya kuaga miili ya watu wa ajali hiyo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Mkoani Kagera 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa pole kwa ndugu wa Marehemu waliojitokeza katika uwanja wa Kaitaba yalipofanyika maombolezo ya kitaifa ya wahanga wa ajali ya ndege ya shirika la Precision, Ajali hiyo ilitokea Novemba 6, 2022. Maombolezo hayo yamefanyika katika uwanja wa Kaitaba - Bukoba Mkoani Kagera Jumatatu 7/11/2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...