Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Young Africans SC wamefuzu makundi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi jumla ya bao 1-0 dhidi ya Club Africain ya Tunisia, mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo bao la Young Africans lilifungwa na Mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kwenye dakika ya 78 ya mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa kwenye dimba la Hammedi Agrebi Olympique - Rades mjini Tunis.
Young Africain imefuzu hatua ya makundi katika Michuano hiyo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2018, sasa hivi imefanya hivyo katika ardhi ya ugenini dhidi ya Club Africain.
Yanga SC wanaunmgana na Simba SC ambao wao wamefuzu hatua ya makundi ya Michuno ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuzitoa timu za Big Bullets ya Malawi na Club De Agosti ya Angola.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...