MKAZI wa Kitunda Mwanagati Jijini Dar es Salaam, Seleman Maziku, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kughushi ridhaa ya mke wake na kujipatia Sh. milioni 140 kwa njia ya udanganyifu.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Yusuph Aboud mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio imedai Desemba 10, mwaka katika mahali pasipojulikana mshitakiwa alighushi ridhaa ya mkewe Scora Bundala.

Katika shtaka la pili inadaiwa siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam mshtakiwa Maziku alijipatia mkopo wa Sh. Milioni 140 kutoka benki ya Stambic baada ya kuwasilisha ridhaa hiyo ya mkewe ya kughushi.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo na kwa mujibu wa upande wa mashitaka, upelelezi katika kesi hiyo umekamilika.

Hakimu Mary alitoa masharti ya dhamana kuwa mshitakiwa ambapo amemtaka kuwa na wadhamini wawili wenye barua watakaotoa pesa taslimu Sh. Milioni 70 kila mmoja ama kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na amerudishwa rumande hadi Desemba 28, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...