Benki ya BancABC Tanzania, ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara imeendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha ya kwamba wanafunzi wanapata elimu katika Mazingira bora na rafiki kwa kukarabati vyoo kwenye shule ya Sekondari ya Dar es Salaam iliyopo katika jijini la Dar es Salaam wilaya ya Ilala. Ukarabati wa vyoo hivyo ambao umegharimu zaidi ya milioni 18 za kitanzania utaweza kufaidisha wanafunzi zaidi ya 600 wa shule hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vyoo hivyo kwa uongozi wa shule ya Sekondari ya Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya BancABC Tanzania Imani John alisema kuwa ukarabati wa vyoo hivyo utaweza kuwafaidisha wanafunzi zaidi ya 600 na hivyo kuwapa nafasi nzuri ya kupata elimu kwa Maisha yao ya baadae, pia hii ni katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutoa huduma bora za kijamii na kuboresha maendeleo ya elimu kwa Watanzania.

Imani aliongeza, ‘Hii sio mara ya kwanza kwa BancABC Tanzania kushiriki katika shughuli za kijamii kama hizi, sisi kama taasisi ya kifedha tunatambua ya kuwa tuna mchango mkubwa katika kusaidia jamii yetu inayotuzunguka hivyo tumekuwa tukijikita katika matukio mbalimbali ya kijamii ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali yetu ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu’.

Aliongeza kuwa BancABC iliona ni vyema kuboresha sekta ya elimu nchini kupitia ukarabati wa vyoo vya shule hii, tunaamini ili mtoto aweze kujifunza vyema lazima tumpatie mazingira rafiki yanayomzunguka hivyo basi tumefanya maboresho ya vyoo 27 Pamoja na system ya maji taka.

‘Benki ya BancABC kama taasisi ya fedha tunafanya juhudi za kusogeza huduma za kifedha ili kuwafikia Watanzania wengi kupitia mawakala zaidi ya 700 tulionao nchi nzima na satellite Zaidi ya 100 katika wilaya mbalimbali Nchini. Tunazo akaunti za kuwainua wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwapatia mikopo ya biashara, pia tuna huduma ya mikopo tunayoitoa kwa wafanyakazi wa serikalini kupitia satellite zetu nchi nzima. Mikopo yetu ina riba nafuu na inapatikana ndani ya muda mfupi sana.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia ukabidhi wa vyoo hivyo, Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mussa Azan Zungu alisema msaada wa kukabarati vyoo hivyo uliofanywa na BancABC Tanzania umedhihirisha uhusiano mzuri uliopo kati ya serikali na sekta binafsi jambo ambalo lilikuwa likinufaisha jamii na ukarabati wa vyoo hivyo utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba uliokuwepo kwa miaka mingi.

Natoa pongezi zangu kwa benki ya BancABC Tanzania kwa kuona umuhimu wa kukarabati vyoo vya shule hii. Tunaelewa na kujua umuhimu wa sekta binafsi na hasa kwenye kuunga mkono juhudi za serikali yetu. Tunawaomba kuendelea kufanya kazi nasi kwani mahitaji ni mengi na kwa kufanya kazi kwa pamoja tutaweza kusaidia jamii yetu’, alisema Zungu.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam Hamad Mwalaba, alisema mchango huo umekuja wakati muafaka kwa sababu ya wingi wa wanafunzi darasani, hivyo ukarabati wa vyoo hivyo utakuwa ni msaada mkubwa sana kwa wanafunzi wetu.

‘Tunatumai ukarabati wa vyoo hivi utaleta mabadiliko makubwa katika ufanisi wa masomo yao pamoja na kuboresha ufaulu wao kitaaluma na pia kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika ujenzi wa taifa,’ aliongeza Mwalimu Mkuu.
Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania Mussa Azan Zungu (kati kati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuashiria kuzindua vyoo vya shule ya Sekondari ya Dar es Salaam ambavyo vimekarabatiwa na benki ya BancABC Tanzania kwa gharama ya Tzs 18 milioni ikiwa ni juhudi za serikali za kuhakikisha ya kwamba wanafunzi wanapata elimu katika Mazingira bora na rafiki. Wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji BancABC Tanzania Imani John, wa pili kulia ni Diwani wa kata ya Gerezani Fatuma Abubakari na kushoto ni Katibu wa CCM Kata ya Gerezani Blandina Sinah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...