LILE Tamasha la Kuku choma litafanyika kesho Msasani Beach Club jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Guru Planet Limited, Nixon Martin alisema tamasha litaanza asubuhi hadi usiku ambako wajasiriamali na wadau mbalimbali watahidhuria tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi.

Martin alisema tamasha hilo litakuwa na matukio kama michezo ya baharini, wasanii wa kudance, kuvuta kamba, utoaji wa zawadi kwa watakaoweza kushinda ubunifu wa biashara hasa ya ufugaji wa Kuku ambao watapatiwa zawadi.
Katika tamasha hilo wamewaalika viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na watendaji wengine kutoka wizara hiyo.

Alisema tamasha hilo litajikita kwenye uelimishaji kuhusu ufugaji ambako wataalam wataeleza taratibu na changamoto huku tukio lingine ni kuunganisha vipaji mbalimbali ambako pia michezo mbalimbali itakuwepo kama kuwashindanisha Kuku wa Simba na Yanga, stand up comedy.

Naye Ofisa Masoko wa Guru Planet, Paul Michael alisema katika tamasha hilo kutakuwa na viingilio vitatu, Shilingi 10,000 ambacho mwingiaji atapewa kuku robo, Shilingi 30000 Kuku nusu na vinywaji huku Shilingi 50000 kuku mzima, chipsi na vinywaji na kiingilio kingine ni Shilingi 100000 mteja atapatiwa kuku mzima, mchemsho, supu na vinywaji.

Aidha Michael alisema wamevialika vyuo vikuu saba vya jijini Dar es Salaam ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Mwalim Nyerere, Chuo Kikuu Kampala (KIU), Chuo cha Fedha (IFM) na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).Mhasibu wa Kampuni hiyo, Halima Waziri wamejipanga kuwasaidia vijana kuondokana na tatizo la ajira.



Mhasibu wa Guru Planet, Halima Waziri akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi kuhusu tukio la Kuku choma festival


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...