Na Leandra Gabriel Fernandez, Michuzi TV

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameagiza kuwepo kwa vifaa vya kuhifadhi taka katika magari ya umma na binafsi ili kutunza mazingira ambayo yameathiriwa na takataka hasa zisizooza (plastiki )

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Mjini Iringa wakati akizindua Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi Mazingira na Utunzaji wa vyanzo vya Maji lililoratibiwa na Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA,) na kueleza kuwa suala la utunzaji mazingira, uhifadhi wa vyanzo vya maji na usafi ni jukumu la kila mmoja.

Amesema, kiwango cha uharibifu wa mazingira kinasabanishwa na tabia watu ikiwemo utupaji taka ovyo, ukataji miti, uchomaji moto misitu, uvamizi holela na uvuvi haramu.

"Pembezoni mwa barabara ni takataka tuu, watu wanatupa taka ovyo...Tumechafua, Tusafishe hivyo magari yote ya usafiri wa Umma na binafsi yawe na vifaa vya kuhifadhi takakata." Amesema.

Pia amesema, kiwango cha uharibifu kimepanda kutoka asilimia 42 miaka ya 80 hadi kufikia asilimia 63 mwaka 2018 na kueleza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele katika utunzaji wa mazingira pamoja na Uhifadhi wa vyanzo vya maji kwa kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kushiriki kwa vitendo.

"Kiwango cha uharibifu kimeleta athari nyingi ikiwemo ukame wa muda mrefu, mvua hazitabiriki pamoja na magonjwa kwa Binadamu, wanyama na mimea...ni lazima tunusuru mazingira yetu ikiwemo ya kimkati ikiwemo mto Ruaha Mkuu....Ukiharibu Mazingira yanalipa kisasi, tumeanza kula jeuri." Amesema Dkt. Mpango.

Aidha ametaka ushirikiano baina ya Serikali, vyama vya siasa, Wanahabari, taasisi za dini na sekta binafsi uendelee ili kufanikiwa katika kampeni ya utunzaji wa mazingira pamoja na Uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Dkt. Mpango amewapongeza wanahabari kwa kuonesha uthubutu katika kuokoa eneo la Ruaha na maeneo mengine na kuwataka kufichua sehemu zenye uharibifu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji lililolofanyika kwenye ukumbi wa Masiti Gangilonga Mkoani Iringa Leo Disemba 19,2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...