Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) imeshiriki Mkutano mkuu wa Taasisi ya Ugavi nchini Kenya (KISM) unaofanyika nchini Tanzania kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 14 hadi Desemba 16, 2022.

Akizungumza Naibu Kamishna wa Sera na Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mpango Alex Araba wakati wa kufungua mkutano huo amesema mkutano huo una tija kwa Tanzania hasa kwa Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi hasa kwa kupata ujuzi ambapo mkutano huo unahusisha Wataalamu kutoka katika nchi za Afrika ya Mashariki hivyo kushiriki kwao ni tija sana.

Pia Araba amewataka washiriki wa mkutano huo kushiriki vyema ili kuweza kuja na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wataalamu wa Ununuzi na Ugavi katika nchi za Afrika Mashariki na kupelekea kuhimarisha Shughuli mbalimbali za ununuzi.

“Kama pia Kenya wameweza kuja Tanzania sasa ni muda muafaka kwa Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) nao kupata nafasi kwenda kufanya mkutano kama huu kwa nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupata uzoefu zaidi na kwakuwa ni funzo naamini PSPTB baada ya hapa watakwenda kujipanga ili wafikie malengo watakayokuwa wamejiwekea” Alisema Araba

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Watalaamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi mesema kutakuwa na majadiliano ya siku tatu kwani PSPTB ndio wenyeji wa Mkutano na kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kupata ujuzi pamoja na fursa mpya katika myororo wa Ununuzi na Ugavi hasa kwenye soko ambalo linatetereka kutokana na mabadiliko ya mbalimbali katika dunia.

Pia amesema wataweza kubadirishana mawazo maana katika mkutano huo kuna Wakenya, Waganda, Rwanda pamoja na wenyeji Tanzania baada ya hapo wataangalia ni kwanamna gani wamejifunza ili baadae ikimpendeza Mwenyezi Mungu waweze kuanza kufanya mikutano kwa kuzunguka kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Naibu Kamishna wa Sera na Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha na Mpango Alex Araba akisoma hotuba ya kufungua mkutano mkuu wa Wataalamu wa Ununuzi wa nchini Kenya uliofanyia Dar es Salaam nchini Tanzania ukiwa umewakutanisha wadau mbalimbali wa Ununuzi kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki inaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo terehe 14 hadi Desemba 16, 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Watalaamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza kuhusu PSPTB inavyoshirikiana na taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo taasisi ya KISM katika kuhimarisha taaluma ya ununuzi na Ugavi wakati wa mkutano mkuu wa mkuu wa Wataalamu wa Ununuzi wa nchini Kenya uliofanyia Dar es Salaam nchini Tanzania.

Rais wa IFPSM Marina Lindic akizungumza kuhusu namna wanavyosimamia taaluma ya Ununuzi na Ugavi kwa nchi wanachama wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Wataalamu wa Ununuzi wa nchini Kenya uliofanyia Dar es Salaam nchini Tanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi wa Nchini Kenya(KISM) John Karami akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Taasisi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam ukihusisha wajumbe kutoka nchini Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KISM, Serah Okumu akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wataalamu wa Ununuzi wa Nchini Kenya uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wakisikiliza hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Wataalamu wa Ununuzi wa nchini Kenya uliofanyia Dar es Salaam nchini Tanzania
Picha za pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...