Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akiwa na viongozi wengine wanaosimamia ujenzi wa Mabweni ya kampasi ya Kisangara Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakitembelea kuona maendeleo ya Mradi huo.
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza katika kikao na Mkuu wa Taasisi ISW,  kamishna wa Ustawi wa Jamii na Wasimamizi wa Ujenzi.

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju Akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Taasisi Dkt. Joyce na Watumishi wengine wanaosimamia mradi wa ujenzi wa Mabweni ya kampasi ya Kisangara Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameridhishwa na maendeleo ya Ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara, Mwanga mkoani Kilimanjaro yanayotarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 104.

Katika ziara yake ya kukagua ujenzi huo, Mpanju amepongeza uongozi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa ujumla kwa namna ambavyo imefanya maendeleo ya kuongeza miundombinu ya Taasisi katika kampasi ya Kisangara ikiwemo madarasa ambayo yamekwishakamilika

Amesema mabweni hayo yataboresha huduma za malazi kwa wanafunzi na hasa wa kike, haya yote yakifanywa ndani ya kipindi cha miaka miwili tu tangu Taasisi hii ikabidhiwe kampasi hiyo ya kisangara.

Sio kwasababu ya fedha pekee, ila ni kwasababu ya maono, uongozi na usimamizi wenu wa karibu ndio maana tunaona maendeleo haya katika kampasi hii, hongereni sana” alisema Naibu Katibu Mkuu Mpanju.

Madarasa mapya yaliyo jengwa katika kampasi ya kisangara yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 370 yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi mapema mwezi huu wa Disemba 2022 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Mh. Dorothy Gwajima, na vile vile kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mabweni unaoendelea ambao umefikia asilimia Hamsini (50) mpaka sasa.

Katika ziara hiyo, Mpanju aliambatana na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Vicensia Kagombora wa Wizara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...