SERIKALI kwa kushirikiana na wadau inatambua umhimu wa kuwa na wanawake viongozi Mahili na kuwekeza Rasilimali katika Usawa wa Kijinsia kama Chachu ya kutokomeza Ukatili wa kijinsia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima wakati akizungumza katika Kongamano la tatu la lililoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia (TGNP), kongamano hilo limefanyika Katika Hoteli ya Hyatty jijini Dar es Salaam leo Desemba 2, 2022. Amesema kuwa Serikali imeridhia Mikataba ya kimataifa na Kikanda inayoweka misingi ya usawa kwa binadamu ikiwemo haki na usawa katika kushiriki kwenye uongozi wa ngazi zote na kutokomeza aina zote za ukatili wa Kijinsia.

Dkt. Gwajima amewaasa wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali kuiendeleza miundombinu ya ambayo imewekwa kubeba ajenda za wanawake katika maeneo mbalimbali nchini iwe inafanya kazi kikamilifu. 

Amesema kuwa iwe ni aibu mwanamke kiongozi kuwepo katika eneo ambalo Ajenda ya wanawake inafifia.

Amesema kuwa kongamano hilo la wanawake linafanyika kama Sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili ambapo Kauli mbiu Kila uhai unathamani tokomeza Mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Dkt. Gwajima amewapongeza TGNP kwa kuwa kinara kwa kuwaandaa wanawake viongozi kwa kupitia Programu ya Ukungwi na Ulezi wa Wanawake Viongozi kwa kupitia.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Lihundi amesema kuwa  Ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na uongozi ni chachu ya kutokomeza ukatili wa Kijinsia.

Pia amewaomba Wanawake Viongozi kuonesha Mfano katika vita dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa sababu Wanafahamu ubaya wa Ukatili wa Kijinsia na wengi wamepitia ukatili huo kwa njia moja ama nyingine.

Pia katika Kongamano hilo wameeleza namna ambavyo uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi unavyochangia Ukatili wa Jinsia pale Wanawake na Watoto wanapotafuta nishati ya Kupikia na Maji. 

Kampeni hii ya kupinga ukatili  hufanyika kuanzia Novemba 25 na kumalizika Desemba 10 ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki 1za wanawake. Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili mwaka huu inaadhimishwa kwa kaulimbiu isemayo “Kila Uhai Una Thamani: Tokomeza Mauaji na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.” 

Na Kongamano la Tatu Mada kuu ni 'Ongeza Rasilimali, Ungeza Ushiriki wa Wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia.'

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya TGNP Gemma Akilimali akitoa taswira halisi ya namna walivyoweza kukabiliana na ukatili wa kijinsia wakati wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), Lilian Liundi akisoma risala kuhusu namna mtandao huo unavyofanya kazi hasa katika kutetea haki za wanawake na watoto pale wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia wakati wa wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Same Anastazis Tutuba akizungumza kuhusu namna wanavyoshirikiana na TGNP katika kupambana na ukatili wa kijinsia pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima kwa ajili ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja mwandamizi wa Amir Abdalah akizungumza kuhusu namna walivyijipanga kushirikia na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kuoinguza ukatili wa kijinsia kwenye jamii wakati wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda  akizungumza kuhusu namna wanavyopambana kuinua watoto wa kike kupitia program ya shirika hilo wakati wa kutambulisha  ya timu ya Masala Princess kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima akiburudika na timu ya wanawake ya Masala Princess iliyochini ya shirika la Childbirth Survival International(CSI) wakati wa wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Burudani zikiendelea
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima akipikea zawadi kutoka kwa Mwenyekitu wa Bodi ya TGNP Gemma Akilimali na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), Lilian Liundi wakati wa kogamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa masuala ya jinsia wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima  alipokuwa anafungua Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya makundi mbalimbali ya kupambana na ukatili wa kijinsia wakati wa Kongamano la Wanawake na uongozi ikiwa na kauli mbiu isemeyo Wekeza Rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika Uongozi ili kutokomeza Ukatili wa Kijinsia wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...