SERIKALI mkoani Ruvuma imekamilisha mradi wa ujenzi wa madarasa 156 pamoja na samani zake katika shule za sekondari yaliyogharimu shilingi bilioni 3.1.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mwezi Oktoba mwaka huu ilitoa fedha za kutekeleza mradi huo mkoani Ruvuma.

“Madarasa yapo tayari kupokea wanafunzi waliochaguliwa kidato cha kwanza Januari 2023”,alisisitiza RC Thomas.

Hata hivyo amesema hayo ni mafanikio makubwa kwa kuwa sasa katika Mkoa mzima shule zote za sekondari za Serikali zina uhakika wa kupokea wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule hizo.

Amesema hakuna kikwazo tena cha uhaba wa vyumba vya madarasa hivyo ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanaripoti bila kukosa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi bilioni 7.7 zilizojenga shule mpya za sekondari 11 mkoani Ruvuma katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022. Amesema uboreshaji wa miundombinu ya elimu umepunguza utoro na kuongeza ufaulu.

Ametolea mfano ufaulu wa mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2021 Mkoa ulikuwa na ufaulu wa asilimia 90.1.

Kulingana na RC Thomas matokeo ya mitihani ya Taifa ya kidato cha sita mwaka 2022 Mkoa wa Ruvuma umefaulisha kwa asilimia 99.9.

Hata hivyo amesema jitihada zinafanyika kuboresha ufaulu wa darasa la saba na kidato cha nne.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kulia mwenye suti akikagua madarasa na samani zake katika Wilaya ya Namtumbo.


Miongoni mwa madarasa ya shule za sekondari mkoani Ruvuma ambayo yamekamilika ujenzi na samani zake yapo tayari kuchukua wanafunzi Januari 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...