Na John Walter-Babati

Katika kusheherekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwake, Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imefanya Bonanza la michezo mbalimbali iliyohusisha wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.

Akizungumzia bonanza hilo mkurugenzi mtendaji David Mulokozi, amesema dhumuni la michezo hiyo ni kuboresha afya zao na kujenga umoja kwa wafanyakazi pamoja na sherehe za kutimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka 2018 ambayo makao makuu yake ni mjini Babati mkoani wa Manyara.

Mulokozi amesema Kampuni ya Mati Super Brands inajivunia kukua na kuajiri watu zaidi ya ya 250 kutoka watu watatu walioajiriwa kampuni ikianza.

Ameeleza kuwa, Kupitia ajira hizo wamegusa maisha ya Watanzania wengi ambao wameweza kuendesha familia zao, kujenga na hata kusomesha.

Mulokozi amesema kilele cha sherehe hizo zitahitimishwa Desemba 31,2022.

Mati super Brands Ltd ni wazalishaji na wasambazaji wa Vinywaji vya Strong Dry Gin, Sed Pinneaple Flavour Gin, Tanzanite na Strong Coffee.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...