Wazalishaji wa zao la viazi na wadau mbalimbali kutoka sekta hiyo mwishoni mwa wiki walikutana mkoani Mbeya, kujadili hali ya sekta ilivyo sambamba na kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Kongamano hilo liliandaliwa na Ubalozi  wa Uholanzi nchini kwa kushirikiana na  Chuo kikuu  na utafiti cha Wageningen na ulifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ambapo pia kulizinduliwa machapisho ya mwongozo wa kilimo cha viazi kwa wakulima.

Liliwakutanisha wataalamu mbalimbali wa kilimo, wataalam wa uzalishaji wa mbegu, wakulima, watunga sera, wafanyabiashara na viongozi wengine wa serikali.

Washiriki walijadili kwa kina nini kifanyike ili kubadilisha sekta ya viazi katika mfumo wa ushirikiano wa  sekta ya umma na binafsi, hali ya sasa ya sekta ya viazi nchini Tanzania pamoja na mbinu bora na matumizi ya mbegu bora na teknolojia ambayo uzalishaji unaweza kuongezeka maradufu na kufungua fursa zilizopo katika sekta hii.

Tanzania na Uholanzi zina Maelewano kuhusu kuendeleza sekta ya viazi. Kupitia Maelewano haya, nchi hizo mbili zimefanya kazi pamoja katika usajili wa mbegu bora za viazi. Juhudi hizo zilisababisha jumla ya aina 16 za mbegu za viazi zilizoorodheshwa kwenye orodha ya TOSCI. Uholanzi imeisaidia TOSCI kutengeneza katalogi ya kwanza ya aina ya viazi ambayo ilizinduliwa. Inalenga kufikisha mawasiliano kwa wakulima na wadau wengine juu ya aina ya viazi iliyotolewa, maelezo yake na juu ya upatikanaji wa mbegu za viazi ili kuboresha upatikanaji wa mbegu bora za viazi. Aina hizi pia zitaongeza mavuno kwa kiasi kikubwa ikiwa mbinu nzuri za kilimo zitafuatwa na kusaidia sekta kuwa na maamuzi ikiwa tayari ina taarifa za kutosha.

Baadhi ya wadau katika sekta walifanya maonyesho pia kuonyesha bidhaa zao. Mkutano uliwakutanisha wadau wa sekta kwa karibu na kuwaunganisha pamoja kwa lengo la ukuzaji wa sekta.

Taasisi zilizoshiriki katika maonyesho hayo ni pamoja na; SNV, Isowelo, HZPC, Agrittera, East Africa Fruits co., TOSCI,TARI, Kilimo trust, MATI-Uyole, Mbeya University of Science & Technology (MUST), Hanse Agrostore International, Yara, Dew limited na Mkombozi Agribusiness.

Akifungua kongamano hilo,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, alisema kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Uholanzi kubuni mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao la viazi nchini.

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mheshimiwa  Wiebe de Boer, alisema Uholanzi inajitahidi kuwawezesha wakulima wa Tanzania ili waweze kubadilisha uzalishaji wao wa mazao ya viazi kuwa biashara ya kibiashara.

“Kwa Uholanzi viazi ni zao muhimu sana. Kiasi cha mbegu za viazi ambazo zinauzwa kwenye nchi za Ulaya asili yake ni nchini humo.  Uholanzi, wakulima wa viazi ni miongoni mwa wachangiaji wakuu katika uchumi. Tumeona jinsi maisha ya wakulima yameboreka kupitia matumizi ya mbegu bora, mavuno yaliyoboreshwa ambayo yanaleta biashara nzuri,” alisema Balozi Wiebe de Boer.

Balozi, Wiebe de Boer, aliongeza kusema kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya kuwa na ardhi kubwa ambapo viazi vinaweza kulimwa karibu kila mahali. Kwa kuzingatia eneo, nchi ikijipanga kimkakati ina uwezo wa kuwa kitovu cha zao la viazi katika kanda hii.

“Maarifa yana nguvu. Uholanzi ingependa kushirikisha ujuzi na utaalamu wake na wakulima wa Tanzania katika safari ya kuboresha uzalishaji wa viazi. Kitabu cha kufundisha uzalishaji bora wa viazi kilichozinduliwa kina maarifa, na mwongozo wa vitendo kwa wakulima” aliongeza Mhe Balozi, Wiebe de Boer.

Kitabu kilichozinduliwa ni cha kipekee sana kwani kimeandikwa kwa lugha nyepesi na ishara ambazo zinawawezesha kuelewaka kwa urahisi na kikitumika vizuri kinaleta mabadiliko kwa wakulima ambao wengi wataendesha kilimo chao kitaalamu.
Kwa kupata taarifa na meaelekezo kwa vitendo kutoka kwa wataalamu wa kilimo, wakulima wataongeza ufanisi na kuwa na uzalishaji endelevu wa viazi. Hatimaye watapata mavuno mazuri.

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mheshimiwa  Wiebe de Boer (Kulia), na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh.Juma Homera (kushoto) wakizindua machapisho ya kutoa elimu ya uzalishaji viazi wakati wa kongamano hilo.


Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Mheshimiwa  Wiebe de Boer (Kushoto), na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh.Juma Homera (kulia) waliungana na wageni waalikwa kuzindua  machapisho ya kutoa elimu ya uzalishaji viazi wakati wa kongamano hilo


Baadhi ya wadau kutoka sekta ya viazi wakipokea machapisho yanayoelekeza kilimo bora cha viazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...