Yametia! Hatimae washindi wa wanne wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wameanza safari hii leo kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu.
Washindi hao wannne Abdallah Tangarisi (Singida), Victor George Mwaifunga (Dar es salaam), Konolia Leonard Hinju (Songea) na Mpoki Wamakimbika (Mbeya) wameondoka jijini Dar es Salaam mchana hii leo wakiambatana na baadhi ya maofisa kutoka benki ya NBC.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari hiyo, Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Kimaryo alisema wakiwa nchini Qatar washindi hao watapata fursa ya kwenda uwanjani ili kushuhudia mechi ya robo fainali ya michuano hiyo kati ya mataifa mawili vinara kwenye mchezo wa soka, Uingereza na Ufaransa.
“Hatimaye maandalizi ya safari ya kuelekea Qatar sambamba na washindi wetu wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar yamesha kamilika na sasa tupo tayari kupanda ndege kuelekea huko kutazama mechi ya robo fainali baina ya Ufaransa na Uingereza. Benki ya NBC tutagharamia gharama zote kuanzia usafiri wa kutoka hapa kwenda Qatar, malazi na gharama zote zitakazohusika katika safari yote huko Qatar” alisema Alina
Kwa mujibu wa Alina, wakiwa huko pamoja na kutazama mechi hiyo washindi hao watapata fursa nzuri ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye mvuto ikiwa ni sehemu ya utalii, hatua ambayo itaongeza radha ya safari hiyo kwa washindi hao.
“Lengo letu ni kuhakikisha washindi wetu wanafurahia siku watakazokuwa huko na ndio maana tutao fursa kwao kuweza kutembelea maeneo yenye mvuto zaidi wakiwa huko ili waweze kufanya utalii pia,’’ aliongeza.
Kabla ya kuanza safari hiyo, washindi hao walipokelewa rasmi jijini Dar es Salaam jana na wenyeji wao benki ya NBC na kutambulishwa rasmi katika hafla fupi ya jioni iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini sambamba na maofisa wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC,Bw Elibariki Masuke.
Wakielezea hisia zao kufutia ushindi wao na safari hiyo, washindi hao walisema imekuwa ni furaha kubwa kwao kwa kuwa hawakutarajia safari hiyo, huku wakiipongeza benki ya NBC kwa kampeni hiyo iliyowawezesha kwenda nchini Qatar kushuhudia mchezo wanaoupenda wakiwa wamelipiwa kila kitu.
“Iliniwia vigumu kuamini kwamba nimeshinda safari hii hadi pale nilipothibitishiwa na maofisa wa benki ya NBC tawi la Mbeya. Nimekuwa mteja wa NBC kwa muda mrefu na nimekuwa nikifurahia huduma zao muda wote ila kwa hili wamenifurahisha sana na ninaahidi kuendelea kuwa balozi mkubwa wa benki hii…nawashukuru sana benki ya NBC,’’ alisema Bi Mpoki Wamakimbika mshindi wa kampeni hiyo kutoka Mbeya.
Maofisa wa benki ya NBC akiwemo Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Kimaryo (kushoto) na Meneja Biashara na Mauzo wa benki hiyo Bi Dorothea Mabonye (Kulia) sambamba na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo wakionesha nyaraka za kusafiria muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC,Bw Elibariki Masuke (kulia) akizungumza na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Hazina na Masoko Benki ya NBC,Bw Peter Nalitolela (wa pili kulia) akizungumza na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru (wa pili kulia) akizungumza na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC,Bw Elibariki Masuke (katikati) akikabidhi nyaraka za kusafiria kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki ya NBC wakitoa neno la shukrani kwa uongozi wa benki hiyo kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki ya NBC wakitoa neno la shukrani kwa uongozi wa benki hiyo kabla kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa wateja Wadogo wa NBC,Bw Elibariki Masuke (wa nne kulia) sambamba na maofisa wengine waandamizi wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla ya washindi hao kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC (mstari wa nyuma) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kampeni ya Jaza Kibubu Tusepe Qatar inayoendeshwa na benki hiyo muda mfupi kabla ya washindi hao kuanza safari kuelekea nchini Qatar kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2022 kati ya Uingereza na Ufaransa itayochezwa Disemba 10, mwaka huu. Hafla ya kuwaaga washindi hao imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...