Katibu Tawala Mkoa wa Pwani  Zuwena Omary  akizungumza na waandishi wa Habari  hawapo pichani kwenye  mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Pwani Ally Hengo akitoa  neno la shukrani baada ya mafunzo hayo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa kwenye mafunzo hayo

Na Khadija Kalili Pwani 
KATIBU Tawala Mkoa wa Pwani,Zuwena Omary  ametoa rai kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani kutumia Kalamu zao kwa weledi na uzalendo katika kuandika babari za mradi wa Shule Bora ambao ni mpango makati katoa elimu Bora kwa atoto wote. 

Amesema hayo leo Disemba 8,2022 Wilayani Kibaha alipokua mgeni rasmi kwenye mafunzo ya siku moja kwa Waandishi wa Pwani. Mradi huo wa Shule Bora umelenga kuiunga mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa wanafunzi wote wa kike na kiume katika Shule za Serikali nchini. 

Amesema mradi huo ni wa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na UK Aid mradi huu utafanya maboresho yatakayowezesha kila mtoto kupata msingi mzuri katika elimu yake ya awali, ili kuitumia fursa kwa kutoa mchango wake katika ukuaji wa nchi na maendeleo yake.

Amesema kuwa mradi huu ni kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK Aid, gharama za mradi zitakuwa na bajeti ya Paundi za Kiingereza Mil.89 , sawa na Sh.za Kitanzania Bil.271 na utafanya kazi katika ngazi zote za mradi. Mradi huu wa Shule Bora utatekelezwa hadi ifikapo mwaka 2027. 

Mradi huu wa Shule Bora una malengo manne ambayo ni kujifunza watoto wote watapata fursa ya kujifunza katika shule. Lengo.la pili ni Kufundisha mfuko wa msaada wa UK Aid utaunga mkono na kuimarisha kazi ya ufundishaji nchini.

Lengo la tatu Jumuishi ambapo itahakiki sha kuwa watoto wote wa kitanzania mashuleni wanakuwa katika mazingira salama na rafiki ili kuwa wezesha kumaliza elimu ya msingi na wana endelea na elimu ya Sekondari na lengo la nne ni kujenga mfumo UK Aid utaunga mkono serikali na kuimarisha ili kupata au kuwa na thamani ya fedha katika utoaji wa elimu katika ngazi zote toka chini hadi ngazi ya taifa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...