MFANYABIASHARA Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mke wake Naomi Marijani n kisha kuchoma mwili wake moto kwa kutumia magunia ya mkaa amedai mahakamani kuwa ameiandikia barua ofisi ya Mwendesha Mashtaka barua ya kukiri kosa hilo mara kadhaa lakini amekuwa hajibiwi.

Aidha amemuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuishughulikia ofisi hiyo kwa kushindwa kumjibu barua zake akidai kuwa amekiri kumuua mkewe Naomi Marijani bila kukusudia.

Mshtakiwa Luwonga amedai hayo leo January 24,2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalila baada ya kesi inayomkabili ya mauaji ya kukusudiwa kuitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Mara baada ya kesi hiyo kuitwa, mshtakiwa Luoga alimuomba Hakimu ampatie japo dakika mbili azungumze kidogo.

Amedai kuna jambo linamshangaza sana na ni la ajabu kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wa upande wa mashtaka wanafanya mambo ya ajabu sana, Rais Dk Samia Suluhu Hassan naomba ushughulikie watumishi hawa kwa sababu nimeshaandika barua ya kukiri kumuua mke wangu Naomi bila kukukusudia lakini hadi leo wananizungusha wana kazi ya kuondoa kesi na kuleta mpya," amedai

Amedai, hata kipindi cha marehemu Rais Dk John Magufuli aliandika barua katika ofisi hiyo ya waendesha mashtaka, lakini hajajibiwa hadi leo.

Hata hivyo Hakimu Rugemalira alimuuliza mshtakiwa kama wakati kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga alikiri kosa hilo kama anavyodai akajibu hakuweza kukiri kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji. Jambo ambalo hata wakili wake, Mohamed Majaliwa alipoulizwa akadai kwamba hakuwahi kukiri.

Mshtakiwa Luwonga aliendelea kudai kuwa Oktoba 21,2020 aliposomewa maelezo ya kesi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alikana kumuua mke wake kwa kukusudia.

Kufuatia hayo, Hakimu Rugemalila akamfafanulia mshtakiwa kuwa kesi za mauaji ziko za aina mbili kuua kwa kukusudia na kuua bila kukusudia na kwamba yeye ameshtakiwa kwa mauaji ya kukusudia.

"Ni kweli hakimu, nimeshtakiwa hivyo lakini mimi sikumuua mke wangu kwa kukusudia ndiyo maana niliandika barua. Serikali ilitoa fedha nyingi kuleta mashahidi, lakini badala ya kesi kuendelea wao wakaiondoa wakanisomea upya shtaka na kudai upelelezi haujakamilika,"amedai Luwonga

Hata hivyo, Hakimu Rugemalira alimtaka mshitakiwa awe na subira kwa sababu wakili wake, Majaliwa amepeleka maombi Mahakama Kuu kwa hiyo wasubiri majibu na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 7,2023.

Awali, Wakili wa Serikali, Mosie Kaima alidai kuwa wapo kwenye hatua za kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu, lakini Wakili Majaliwa akadai, wamefungua maombi katika mahakama hiyo ili kuangalia uhalali wa kesi mpya iliyofunguliwa.




Katika kesi hiyo mshitakiwa Luwonga anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani na kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...