Na SALMA AMOUR, TANGA

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga kimetoa Rai kwa viongozi wote wa CCM kuwapa kipaumbele wazee na kuheshimiwa ambapo wao ndio chimbuko la kizazi kilichopo kwenye jamii Ili kupata mawazo kwao na viongozi wote wa dini katika kuleta maendeleo kwenye jamii yetu.

Ameyasema hayo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM ) mkoa wa Tanga kwenye ofisi za chama CCM mkoa Ili kuomba baraka zao katika kuanza kazi rasmi za chama, Mwenyekiti Rajabu amesema wazee na viongozi wa dini wanastahiki kuheshimiwa Ili uongozi uweze kuwa na baraka na endapo chama kitazidiwa kimajukumu wataomba muongozo kutoka kwao.

"Wakati wa ujana wenu nanyi mliwasaidia Marais wetu katika awamu tofauti kwa nyakati tofauti,kwa nafasi tofauti kwa kukuza uchumi wa nchi wakulima walilima kwenye Taifa letu,wengine mulifanya biashara, waliofanya kazi ofisini kama ma DED,RC,wakuu wa wilaya na kadhalika, Bado mlitoa mchango mkubwa sana kwenye Taifa letu". Alisema Mwenyekiti Rajabu.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Rajabu aliezela kuwa lazima wazee wapewe kipaumbele katika huduma kwenye maeneo yote hasa wanapokwenda hospitalini Ili kupata matibabu Huku akiahidi kulisisamia suala Hilo.

" Kwa hiyo nayasema haya sio kwa kubahatisha, ndio yaliyopo kwa sababu watu wengine wanaona kuwa chama kinasinzia,hakichukui hatua yeyote ndugu zangu chama ndio kimeiweza serikali madarasani Tena kina meno na yanang'ana kama ya mamba,Asie amini ajaribu aone, lengo ni kumsaidia Raisi wetu ambae ndio Mwenyekiti wa CCM Taifa daktari Samia suluhu Hassan ,kwa hiyo wazee na viongozi wote wa dini lazima waheshimiwe na kupata haki zao za msingi na nitafuatilia hatua kwa hatua".. Mwenyekiti Rajabu.

Aidha aliwataka wazee na viongozi wa dini kuwafungisha vyema watoto maadili mema ambayo ndio Changamoto kuwa katika kizazi Cha Leo maadili yanaporomoka siku Hadi siku.

Kwa upande Wake Ustadh maalim bin umary kutoka taasisi ya Rashaad lslamic group alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoa kutembelea katika kata zote Ili kujua Changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii ya Tanga ikiwemo ujenzi wa barabara katika maeneo yenye uhitaji.

Nao pia baadhi ya viongozi wengine wa dini wamemuomba Mwenyekiti kuwa karibu na watu wote pasipo kuangalia dini,kabila na kipato Ili kuweza kufikia lengo kililokusudiwa la kuleta maendeleo kwenye mkoa wa Tanga.

Vile vile baadhi ya wazee wa Tanga walishukuru serikali ya Tanzania kuwajali kwa kuwapatia fursa muhimu ya kuzibainisha Changamoto walizo nazo kwenye jamii Ili kuleta matokeo chanya na kuahidiwa kutimiza kwa wakati uliokusudiwa.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdul Rahman akizungumza jambo na wazee pamoja na viongozi wa dini wa mkoa wa Tanga.
Wazee wa mkoa wa Tanga walisikiliza maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman katika kikao Cha kujadili maendeleo ya mkoa wa Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...